"Ningependa kuwa kitandani nawe" Huddah Monroe amwambia Jux huku huba lao likinoga

Muhtasari

•Wengi wameanza kuamini kuwa wasanii hao wawili huenda wachumbiana kwani tayari wameonyesha dalili za kuaminika.

•Huddah alimsihi msanii huyo kushikilia mpango wao wa kuenda kilabu ili kwanza waweze kutulia pamoja nyumbani.

Huddah Monroe na Juma Jux
Huddah Monroe na Juma Jux
Image: INSTAGRAM// JUMA JUX

Staa wa Bongo Juma Jux na mwanasoshalaiti maarufu kutoka Kenya Huddah Monroe wameendelea kuwa gumzo kuu mitandaoni kufuatia vitendo vyao pamoja vya hivi majuzi.

Wengi wameanza kuamini kuwa wasanii hao wawili huenda wachumbiana kwani tayari wameonyesha dalili za kuaminika.

Kwa sasa Huddah yupo nchini Tanzania, siku chache tu baada ya kuahidi kwenda huko kukutana na staa huyo wa Bongo. Akitoa tangazo hilo mwanasoshalaiti huyo alidokeza kuwa lengo la ziara yake ni kushiriki mapenzi na Jux.

"Nilikuja kwa ajili ya hilo," Huddah aliwahakikishia waandishi wa habari baada ya kutua katika uwanja wa ndege.

Jux alimlaki kipusa huyo ambaye ametambulisha kama 'malkia wangu' kisha kuandamana naye hadi nyumbani kwake.

Baadae Jux alipakia video inayoonyesha akiwa amebarizi na mwanasoshalaiti huyo nyumbani kwake. Wawili hao walionekana kuwa na kipindi kizuri pamoja na hata hawakuogopa kubusu mbele ya camera.

Katika video hiyo Jux alimuuliza kipusa huyo kuhusu mpango wao wa jioni. Ingawa wawili hao walikuwa wameratibiwa kutumbuiza klabuni Huddah alisema angependa sana kusalia kitandani na mwanamuziki huyo.

"Mimi na mpenzi wangu tumetulia tu.. sijui, ningependa kuwa kitandani na wewe," Huddah alimwambia Jux

Huddah alimsihi msanii huyo kushikilia mpango wao wa kuenda kilabu ili kwanza waweze kutulia pamoja nyumbani.

"Ukiwa na Jux sasa unaenda wapi? Kwa nyumba nzuri hivi, natulia" Alisema Huddah.

Mwishowe wawili hao walikubaliana kuenda katika klabu cha Elements jioni hiyo huku wakiwasihi mashabiki wao kujitokeza.

Uvumi kuwa mpenzi huyo wa zamani wa Vanesaa Mdee anachumbiana na Vera ulianza kutanda baada ya picha yao wakibusu wakiwa ndani ya gari kusambaa mitandaoni.

Hivi majuzi Jux aliachia kibao 'Simuachi' ambapo Huddah ndiye alikuwa video vixen mkuu.