Nusu uchi? Mtindo wa mavazi wa Akothee akitumbuiza nchini Sweden wazua hisia mseto (+picha)

Akothee alionekana akiwa amevalia vazi jeusi lenye utata ambalo lilifunika tu sehemu ya juu ya mwili wake.

Muhtasari

• Akothee alitumia sehemu ya maelezo ya chapisho hilo kujitetea na kuweka wazi kuwa yeye si mfano wa kuigwa kwa mtu yeyote.

•Baadhi ya Wakenya walionekana kutoridhishwa na vazi lake na kwa hilo wakamshambulia huku wengine wakionekana kumtetea.

Akothee akitumbuiza nchini Sweden
Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Mwanamuziki wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee amezua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mtindo wake wa mavazi wakati alipokuwa akitumbuiza mbele ya mashabiki wake jijini Stockholm, Uswidi wikendi.

Jumatatu jioni, msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 alishiriki na mashabiki wake mtandaoni baadhi ya picha zake akitumbuiza jukwaani katika nchi hiyo ya Ulaya, ambapo alionekana akiwa amevalia vazi jeusi lenye utata ambalo lilifunika tu sehemu ya juu ya mwili wake.

Kabla hata wanamtandao hawajatoa maoni yao kuhusu picha hizo, jambo ambalo bila shaka lilitarajiwa, Akothee alitumia sehemu ya maelezo ya chapisho hilo kujitetea na kuweka wazi kuwa yeye si mfano wa kuigwa kwa mtu yeyote.

“Huyu Ndiye AKOTHEE MSANII. Mwimbaji, mburudishaji na sio aina yako ya mfano. Msanii huyu Akothee ana soko lengwa tofauti leo. Weka mdomo wako mahali pesa zako zilipo. Akiwa na Dj Ike anayetafutwa zaidi. SWEEEEEDEN ilikuwa MOTO. Asante sana. HATUA NYINGINE,” Akothee alisema chini ya picha hizo.

Katika picha hizo, mama huyo wa watoto watano alionekana akiwapa mashabiki wake shoo ya kusisimua kwa huku wanadensi wa kike wakicheza nyuma yake.

Wanamitandao waliotoa maoni kwenye chapisho hilo walionekana kuvutiwa zaidi na vazi lake jeusi lililofunika tu sehemu yake ya juu ya mwili wake. Ukaguzi wa karibu wa picha hizo hata hivyo unaonyesha kuwa miguu na mapaja yake, licha ya kuwa yalionekana, yalifunikwa na nguo nyepesi.

Baadhi ya Wakenya ambao walitoa maoni yao walionekana kutoridhishwa na vazi la mwimbaji huyo na kwa hilo wakamshambulia huku wengine wakionekana kumtetea wakisema pia wanariadha na watu wengine mashuhuri wa kimataifa huwa wanaburudisha wakiwa wamevalia mavazi yasiyofunika mwili wote na huwa hawahukumiwi.

Tazama baadhi ya maoni kutoka kwa Wakenya;

Anyanya Peter: I don’t knoe what makes women artists naked in the music industry.

Akothee alijibu: Female artist not women artist. Music is for the eye not the ears, that’s why we have audio visual, punda

Ayoo Pressy: Madam Boss respect your children and workers.

Dorothy Wanjiku Wambui: Waah hizi ni gani Madam Boss.

Peter Kinuthia Muchene: Kamon gal, shayki wat yua mamaa gav yuu. Don fi wat jelas pipo will say. We sapot yuu sanaaa.

Kun Kennedy Ayzzac: Nothing is wrong here anyone who has watcheD Beyonce performance of late.

Maureen Karimi: Different event, different crowd and of course different outfit!! Simple and clear.