Paula amuonya vikali Harmonize baada ya kufichua alimtongoza kabla hajachumbiana na mama yake, Kajala

Konde Boy amedai kuwa mwanamitindo Paula Kajala hamchukii bali alipatwa na wivu tu.

Muhtasari

•Konde Boy alidai kuwa Paula alimtafuta kupitia kaka yake wa kambo akiwa na matumaini ya kuwa na uhusiano wa karibu naye.

•Paula alimtaka bosi huyo wa Konde Music Worldwide kumuacha na kumwangazia mwanamke anayedaiwa kupata naye mtoto.

amedai kwamba Paula alipatwa na wivu baada ya yeye kuchumbiana na mama yake.
Harmonize amedai kwamba Paula alipatwa na wivu baada ya yeye kuchumbiana na mama yake.
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amedai kuwa mwanamitindo Paula Kajala hamchukii bali alipatwa na wivu tu.

Katika taarifa yake ndefu kwenye Instagram, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alidai kuwa mrembo huyo mwenye umri wa miaka 20 alimtafuta hata kabla hajaanza kutoka kimapenzi na mama yake Frida Kajala.

Konde Boy alidai kuwa Paula alimtafuta kupitia kaka yake wa kambo akiwa na matumaini ya kuwa na uhusiano wa karibu naye.

“Ki ukweli kabisa hanichukii (Paula). 2017 alinitafuta kupitia mdogo wake wa kiume POL wa baba mmoja. Aliniambia dada yangu anataka kuongea nawe, huu ndio ukurasa wake wa Instagram. Nikusaidie tum binti yupo Instagram tangu 2017, mimi na machizi wenzangu tunajua!! Wee unajua kaanza mwaka juzi,” alisema Harmonize wakati akimjibu aliyekuwa mpenzi wake, Kajala Masanja.

Mwimbaji huyo wa kibao ‘Single Again’ alidai kuwa Paula alianza kuumia na kusumbuliwa na wivu baada ya kurudi nyumbani alipomaliza shule maliza shule na kugundua kuwa mama yake alikuwa amezama kwenye dimbwi nzito la mapenzi naye na walikuwa pamoja.

”Niliongea naye na akanipa namba yake, na akasema usimuambie mama nyingi sana. Sikumzingatia pia alikuwa mtoto sana na ukiizingatia alikuwa shule bado. Baada ya miaka miwili anakuta penzi limekolea, nakujali, nakuhudumia, kila unachotaka nakupatia na hata yeye pia nampa atakacho kama binti yangu akaanza kuumua nini hivi!! Alitamani awe yeye, alianza kuomba pesa zaidi,” aliamuandikia Kajala.

Konde Boy alisema licha ya yote aliendelea kumheshimu mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20 hadi alipogundua kuwa Kajala alikuwa akitumia simu yake kuzungumza na wanaume wengine.

Pia alidokeza kuwa alishangaa sana baada ya madai kuwa alikuwa akijaribu kumtongoza Paula kuibuka na kudai kuwa hapo awali walikuwa wamewahi kushiriki mazungumzo kama hayo mara nyingi bila shida yoyote.

“Baada ya kugundua nyinyi ni marafiki tu mnanichora ikabidi nianze kumjibu kwa nguvu zoteee. Kwa hiyo hata suala la zima taaa nashangaa tu siku ile ilikuwaje ikiwa tulishaingea mara kibao tuu maongezi ya namna ile,” alisema.

Katika majibu yake, Paula alimtaka bosi huyo wa Konde Music Worldwide kumuacha na kumwangazia mwanamke anayedaiwa kupata naye mtoto.

“Hii namba usiiguse kabisa!!! Sitaki kukuvunjia heshima. Siko kwenye mood kabisa leo. Achana na mimi. Achana na mimi. Kama wewe unavuta b*ngi mdomo mimi navuta m*tak*ni. Sasa tulia,” Paula alijibu.