Pritty Vishy afichua kwa nini hajaanza kuishi na mpenzi wake mpya

Pritty Vishy aliweka wazi kuwa bado hayuko tayari kupata watoto na mwanamuziki huyo.

Muhtasari

•Pritty Vishy alifichua kuwa mwanzoni alisitasita kujitosa kwenye mahusiano na Madini baada ya kugundua kuwa ana mke mwingine.

•Vishy aliweka wazi kuwa bado hayuko tayari kupata watoto na mwanamuziki huyo.

Image: INSTAGRAM// MADINI CLASSIC

Aliyekuwa mpenzi wa Stivo Simple Boy, Pritty Vishy amesisitiza kuwa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Madini Classic.

Akiwa kwenye mahojiano na Eve Mungai, Vishy alifichua kuwa alikuja kujuana na mwanamuziki huyo kutoka Pwani mwezi Mei.

Alidai kuwa Madini mwanzoni Madini alitaka kumshirikisha kwenye video ya wimbo wake kabla ya hisia za kimapenzi kuwaingia.

"Nilimpenda kutokana na jinsi  ambavyo ananitunza. Kusema kweli sijawahi kushuhudia kitu kama ambacho Madini alikuwa akinifanyia. Hii ilikuwa tofauti nikasema acha nijaribu," Vishy alisema.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 20 hata hivyo alisitasita mwanzoni baada ya kugundua kuwa Madini ana mke mwingine.

"Aliniambia nisijali. Niliambia mama yangu akaniambia niwe makini ikiwa ameoa... Najua ako na mke Mombasa. Mimi husema ni heri uniambie kuwa kuna mtu mwingine badala ya kunicheza," Alisema.

Vishy pia aliweka wazi kuwa hajawahi kukutana wala kuzungumza na mke huyo mwingine wa Madini.

Katika kipindi cha Maswali na Majibu, mpenzi huyo zamani wa Simple Boy alifichua kuwa hana mpango wa kuishi na mpenziwe.

"Naishi pekee yangu, sina mipango ya kuhamia mahali pamoja na yeye juu weeh kumbuka tuko wawili na tukihama pamoja nitapata ujauzito, kitu sitaki buana. Mnajua huwa napenda tendo la ndoa sana," Vishy alimjibu shabiki aliyehoji ikiwa tayari amehama kwa wazazi wake na kuanza kuishi pamoja na Madini.

Vishy pia aliweka wazi kuwa bado hayuko tayari kupata watoto na mwanamuziki huyo. Hata hivyo alidokeza huenda akapata mtoto naye siku za usoni.

Kipusa huyo pia amempongeza mpenzi wake wa zamani Stivo kwa kumvisha mpenziwe wa sasa pete ya uchumba.

Wikendi Stivo alipiga hatua ya kumvisha pete ya uchumba mwanadada anayedaiwa kuwa mpenzi wake mpya.

"Kusema kweli nina furaha kwa ajili yao. Mimi nina furaha sana kwa ajili yake (Stivo) kwa sababu ata nilimove on. Kila mtu amemove on," Vishy alisema katika mahojiano na Eve Mungai.

Vishy alimshauri mpenzi huyo wake wa zamani kuwa makini kuhusu masuala ya mahusiano na ndoa.

Pia alimsihi kuendeleza uhusiano mzuri wa kirafiki naye licha ya kuwa walitengana miezi kadhaa iliyopita.

"Ningependa awe rafiki yangu. Juu tuliachana haimaanishi tunafaa kuwa maadui. Huwezi kujua huko mbele tutasaidiana vipi. Ningependa awe rafiki yangu na apate mtu bora zaidi," Alisema.

Vilevile alimshauri  awe anamdekeza mchumba wake wa sasa na kumuonyesha mapenzi jinsi ambavyo wanadada hupenda.