Mtangazaji mashuhuri Lulu Hassan amefichua kuwa yeye na mume wake Rashid Abdalla ni wazazi tofauti kabisa.
Akiwa kwenye mahojiano na SPM Buzz, Lulu alifichua kuwa mumewe ni mzazi mkali kwa watoto wao ilhali yeye sio mkali.
Lulu alifichua kuwa watoto wao mara nyingi humuona yeye kuwa mwenye kufikika zaidi kuliko mumewe.
"Hata watoto wakitaka kitu, ni heri waniongeleshe ama waambie mtu aniambie mimi ndio nitawapea, baba ni mkali. Yeye huwachapa. Ni jambo nzuri kwa sababu sote tungekuwa kama mimi sijui tungekuwa na watoto wa aina gani," Lulu alisema.
Msomaji huyo wa habari katika alisema Rashid ni mtu ambaye anapenda kutia adabu kwa watoto wao.
Alifichua imetokea mara nyingi ambapo mumewe ambaye pia ni mtangazaji mwenzake amewaadhibu watoto wao hadi akahisi amekuwa mkali zaidi.
"Rashid ni mtu wa nidhamu. Huenda watu huona Lulu ni mkali na Rashid ni mwepesi, ni kinyume kabisa," Lulu alisema.
Lulu pia alifichua kuwa mumewe ni mtu mwenye busara sana na ambaye anajua kutatua shida kwa urahisi.
"Ako na maarifa. Na sio eti Rashid ni mtu ambaye hupenda kusoma,naweza kuambia. Lakini ukamuuliza swali ata usiku atajibu," Alisema.
Aidha mtangazaji huyo alipuuzilia mbali madai kuwa Rashid alikuwa hohehahe walipokutana na ilhali yeye alikuwa amejizolea utajiri kiasi tayari.
Lulu alifichua kuwa yeye na mumewe walikuwa wanapokea mshahara sawa wa Ksh 5,000 wakati walipokutana.