Samidoh kwa ukali baada ya kuulizwa sababu ya kumficha sana mpenzi wake, Karen Nyamu

Samidoh alisema maneno makali kwa mwanamtandao huyo na kushangaa kwani huwa hana kazi ya kufanya.

Muhtasari

•Shabiki alimshutumu Samidoh kwa kumficha sana mpenzi wake katika moja ya chapisho zake kwenye mtandao wa Facebook.

•Katika miezi kadhaa iliyopita, Samidoh ameonekana mara nyingi pamoja na Karen Nyamu, ambaye amezaa naye watoto wawili.

Samidoh.
Image: FACEBOOK.

Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh alitoa jibu kali baada ya shabiki mmoja kumshutumu kwa kumficha sana mpenzi wake katika moja ya chapisho zake kwenye mtandao wa Facebook.

Mwimbaji huyo alikuwa amechapisha chapisho lililokusudiwa kutangaza show alizopangiwa kufanya mjini Nyeri na Juja wakati shabiki huyo alipomuuliza kwa nini hakumtaja mpenzi wake.

Mtumiaji huyo wa Facebook aliyetambulika kama Phillis Mbuthia alimshutumu staa huyo wa Mugithi kwa kuficha mpenzi wake na kutojivunia mahusiano yao hadharani.

"Mbona hujamtag babe?? Hakii unamfichanga..," Phillis Muriithi alitoa maoni yake.

Katika majibu yake kwa lugha ya Kikuyu, baba huyo wa watoto watano alisema maneno makali kwa mwanamtandao huyo na kushangaa kwani huwa hana kazi ya kufanya.

"Wee nawe no kuha*wo ciugo guuku kai utakoragwo na wa gwika?" Samidoh alisema.

Kumaanisha: Wewe nawe kazi yako ni kuropokwa maneno tu huku, kwani huwa huna kazi ya kufanya?

Makumi ya wanamitandao ambao walipata kuona jinsi mwanamuziki huyo alivyojibu kwa ukali maoni hayo walionekana kufurahishwa na kucheka nayo.

Katika miezi kadhaa ambayo imepita, Samidoh ameonekana mara nyingi akiwa pamoja na mpenzi wake Karen Nyamu, ambaye amezaa naye watoto wawili.

Wawili hao walianza kuonekana sana wakiwa pamoja mapema mwaka huu baada ya mke wa Samidoh, Edday Nderitu kuondoka nchini Kenya kuelekea Marekani ambako amekuwa akiishi na watoto wao watatu. Ingawa mwimbaji huyo huwa hamposti sana mama huyo wa watoto wake wawili kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, Karen Nyamu kwa upande wake anaonekana kujivunia sana uhusiano wao na kawaida huwa haoni haya kuonyesha picha na video zao wakiwa pamoja kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Image: FACEBOOK// SAMIDOH

Mwezi Julai, Edday Nderitu alitangaza kutengana na Samidoh na kuweka wazi kuwa alimuacha  ili awe na mwanamke ambaye alionekana kumtaka zaidi.

"Wacha nifafanue mambo machache ambayo yalishirikiwa mtandaoni na sio sahihi. Siko kwenye ndoa ya wake wengi, kama ilivyoelezwa nilimuacha mume kwa yeyote aliyemhitaji zaidi,” Edday alisema kupitia Facebook.

Aliongeza, "Nilifanya uamuzi wa kujiondoa mimi na watoto wangu kutoka kwa mazingira hayo yenye sumu, haswa binti yangu kijana ambaye kwa bahati mbaya anapokea moja kwa moja tabia isiyoaminika iliyoonyeshwa."

Edday alisema hayo baada ya Karen Nyamu kudai kuwa Samidoh na Edday bado wako katika uhusiano mzuri na huwa wanazungumza.

Katika mahojiano na na Ala C kwenye kipindi cha Reke Ciume na Ene, seneta Nyamu alifichua kuwa Edday ambaye kwa sasa anafurahia wakati na familia yake nchini Marekani bado huwa anawasiliana na Samidoh na akadai kwamba hawezi kwenda popote kwani muungano wao hauwezi kuvunjika kwa urahisi.

“Mambo mnayoyaona kwenye mitandao ya kijamii mtashangaa sana, kuna baadhi ya miungano imetoka mbali sana. Labda hajui kwamba haendi popote, lakini najua kwa sababu miungano mingine si rahisi kukatika,” alisema.

Nyamu alidokeza kuwa mpenzi wake Samidoh na mkewe wa kwanza wamechukua mapumziko lakini bado wako katika uhusiano mzuri.

“Huwa naskia wakiongea, wako sawa sio vile mnafikiria. Hata watoto wanaongea naye kupitia simu yake. Kwa ground hakutawahi haribika,” alisema.

Seneta huyo alisisitiza kuwa yeye si mharibifu na akadokeza kuwa kuna mambo makubwa yatajidhihirisha katika siku zijazo.