Sijafanya mapenzi kwa miezi mitatu- Harmonize azungumzia maisha baada ya kuachwa na Kajala

Mwimbaji huyo amejivunia maisha ya kuwa single.

Muhtasari

•Harmonize amedokeza kwamba mara yake ya mwisho kufurahia tendo la ndoa ni alipokuwa kwenye mahusiano na Kajala.

•Harmonize hajaonyesha majuto yoyote ya kuwa bila mpenzi sasa kwani anadai hilo limemfanya kuwa na nguvu zaidi.

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amedokeza kwamba mara yake ya mwisho kufurahia tendo la ndoa ni wakati alipokuwa kwenye mahusiano na muigizaji Frida Kajala Masanja.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Ijumaa, Konde Boy aliweka wazi kuwa hajashiriki mapenzi kwa miezi mitatu sasa.

Hata hivyo, hajaonyesha majuto yoyote ya kuwa bila mpenzi sasa kwani anadai hilo limemfanya kuwa na nguvu zaidi.

"Maisha ya kuwa single yanakufanya kuwa na nguvu.Miezi mitatu sijawahi kushiriki mapenzi. Najua hamuwezi kuamini hili," alisema kwenye video yake akimuinua mwanamke asiyejulikana na kufanya naye mazoezi.

Mwimbaji huyo aliwapa changamoto wanaume walio kwenye mahusiano kuwainua wapenzi wao kama alivyomuinua mwanadada huyo.

Kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja ambao umepita, bosi huyo wa Kondegang amekuwa akiweka wazi kwamba hayupo kwenye mahusiano yoyote na kuonyesha waziwazi jinsi anavyofurahia maisha ya kuwa single.

Mapema mwezi huu alisema kwa sasa anajipatia muda usiojulikana wa mapumziko kabla ya kujitosa kwenye mahusiano mapya.

"Msijali, hivi karibuni nitapata mtu na mtamjua!!," alisema.

Staa huyo wa Bongo alidokeza kwamba alipitia masaibu mengi mno wakati akiwa katika mahusiano yake ya awali.

Alionekana kuwakashifu wakosoaji na kuwataka wasite kumhukumu kwa kuwa hawana ufahamu wowote wa aliyopitia.

"Wasikuone na kidem tuu!! Hivi mnajua niliyo yapitia," aliandika.

Kajala  alithibitisha kutengana na mwimbaji huyo mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuchumbiana naye kwa takriban miezi saba. 

Ingawa hakuweka wazi kilichowatenganisha, alibainisha kuwa hakubeba kinyongo dhidi yake licha ya mahusiano kugonga mwamba.

Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala alisema mwezi Desemba.

Mama huyo wa binti mmoja aliweka wazi kwamba alikuwa tayari kupiga hatua nyingine baada ya mahusiano kusambaratika.

Katika taarifa yake, Harmonize alibainisha kuwa kuna nafasi kubwa ya upendo ndani ya moyo wake uliovunjika mwaka jana.

"Upendo una nafasi kubwa sana kwenye kichwa changu. Ndio maana napenda watu kuliko pesa. Unaweza hisi mjinga flani. Kwa sasa niko single. Nataka tu kuchukua muda wangu Inshallah," alisema.