"Sijali!" Carrol Sonie azungumzia ex wake Mulamwah kupata mtoto na mpenzi wake mpya

Sonie alidokeza kuwa hajali mzazi mwenzake na mpenzi wake wa sasa kukaribisha mtoto pamoja.

Muhtasari

•Carrol Sonie alijibu kwa kejeli baada ya mashabiki kufurika katika akaunti zake za mitandao ya kijamii kufuatia habari za kuzaliwa kwa mtoto wa Mulamwah.

•Mashabiki walijaza akaunti ya Sonie na habari kuhusu kuzaliwa kwa mtoto wa Mulamwah, pengine kwa nia ya kumkera zaidi muigizaji huyo.

amewajibu wanamitandao kuhusu kuzaliwa kwa mtoto wa pili wa Mulamwah.
Carrol Sonie amewajibu wanamitandao kuhusu kuzaliwa kwa mtoto wa pili wa Mulamwah.
Image: HISANI

Mtayarishaji wa maudhui Caroline Muthoni Ng’ethe almaarufu Carrol Sonie alijibu kwa kejeli baada ya mashabiki kufurika katika akaunti zake za mitandao ya kijamii kufuatia habari za kuzaliwa kwa mtoto wa pili wa mchekeshaji Mulamwah siku ya Jumamosi.

Wikendi iliyopita, Mulamwah na mpenzi wake wa sasa Ruth K walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza pamoja, Oyando Jr almaarufu Kalamwah, na kuibua shangwe na msisimko mkubwa kutoka kwa mashabiki wao.

Huku habari za kuzaliwa kwa Oyando Jr  zikienea kama moto wa msituni kwenye mitandao ya kijamii, kundi la wanamtandao hata walichukua hatua ya kumchokoza mpenzi wa zamani wa mchekeshaji huyo, Carrol Sonie kwa kum’tag na kumtumia jumbe kuhusu habari hizo.

“Mbona nyinyi nyote mnajaa kwenye DM zangu?” Sonie alilalamika kupitia Facebook.

Makumi ya watumiaji wa Facebook waliendelea kufurika katika sehemu ya maoni ya chapisho la Sonie na kuijaza na habari kuhusu kuzaliwa kwa mtoto wa pili wa mchekeshaji Mulamwah, pengine kwa nia ya kumkera zaidi mama huyo wa binti mmoja zaidi.

Kisha muigizaji huyo alitoa maoni akiwajibu mashabiki hao huku akidokeza kuwa hajali mzazi mwenzake na mpenzi wake wa sasa kukaribisha mtoto pamoja.

"Je, ninaonekana kama ninajali?" aliandika.

Mashabiki walijibu kwa hisia mseto huku baadhi wakionekana kusherehekea kuzaliwa kwa mtoto wa kiume wa Mulamwah, wengine wakimchokoza Sonie zaidi huku wengine wakionyesha sapoti yao kwa mama huyo wa mtoto mmoja wa kike.

Mchekeshaji David Oyando almaarufu Mulamwah na mpenzi wake Ruth K walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza pamoja siku ya Jumamosi

Wakati akitangaza habari hiyo njema, Mulamwah alieleza dhamira yake kubwa katika kujenga kumbukumbu na mwanawe.

“MUNGU NI MKUU , hatimaye kijana wetu yuko hapa , mrithi yuko hapa , MFALME yuko hapa - @oyando_jnr aka kalamwah, karibu duniani mwanangu, ni hisia nzuri zaidi ulimwenguni hatimaye kukuona na kukushikilia. siwezi kusubiri sisi kukua na kufanya kumbukumbu pamoja, "alisema.

Pia alimtambua mzazi mwenzake Ruth K, na kumshukuru kwa kumpa mtoto wake wa pili na kuwa naye kila wakati.

"Asante sana @atruthk kwa zawadi hii nzuri na ya kushangaza, asante kwa kuwa karibu nami kila wakati," alisema.

Aliongeza, “Ninahisi mzima tena, nahisi kurejeshwa, nina furaha , familia sasa zina furaha dunia nzima ina furaha , ♥️♥️ . Nakutakia maisha marefu na yenye afya tele kijana wangu na kila la kheri ulimwenguni. baraka tele. Karibu KALAMWAH !! maisha marefu oyando.”