logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Siko sawa!" Muigizaji Baha avunja kimya baada kudaiwa kumlaghai nesi, kuwa na tatizo la kamari

Baha aliendelea kufichua kuwa anauza akaunti yake ya Instagram na ya TikTok

image
na Radio Jambo

Yanayojiri03 June 2023 - 06:30

Muhtasari


•Judy alidai Baha alimfikia akililia msaada huku akidai alikuwa akikabiliwa na matatizo ya kifedha na familia yake  ilikuwa inakaribia kufurushwa 

•Georgina alifutilia mbali madai ya kufurushwa kutoka kwa nyumba na akamfichulia kuwa muigizaji huyo anakabiliwa na tatizo la kamari. 

•Baha na Georgina wameacha kufuatiliana kwenye mtandao wa Instagram, dokezo kwamba heunda mambo sio mazuri kabisa nyumbani.

Muigizaji wa zamani wa kipindi cha Machachari Tyler Mbaya almaarufu Baha anakabiliwa na tuhuma nzito ya ulaghai baada ya mwanamke Mkenya anayeishi Marekani kumshtumu kwa madai kwamba alimdanganya ili kupata msaada wa kifedha.

Siku ya Ijumaa, mwanamke kwa jina Nurse Judy aliibua madai kuwa baba huyo wa mtoto mmoja alimfikia kupitia mitandao ya kijamii akililia msaada huku akidai kwamba alikuwa akikabiliwa na matatizo ya kifedha na familia yake ndogo ilikuwa inakaribia kufurushwa kutoka kwa nyumba yao ya kupanga.

Alidai kwamba mwigizaji huyo alimuomba dola 400  lakini akamtumia dola 150 pekee ambapo aliendelea kumuomba zaidi.

“Baada ya kumtumia dola 150 ambazo hata hakuzithamini, alianza kutuma  sauti za huruma, akizungumzia kutokuwa na wazazi na marafiki wa kugeukia isipokuwa nesi Judy cheeii. Aliendelea kupiga simu, nikawa naudhika. Nilienda kwenye ukurasa wa mkewe ili kuangalia kama huenda akaunti yake ilidukuliwa na labda alitangaza. Lakini nilipofika huko nililazimika kwenda DM," Judy alisema kwenye Instagram.

Alifichua kuwa mpenziwe Baha, Georgina Njenga alifutilia mbali madai ya kufurushwa kutoka kwa nyumba na akamfichulia kuwa muigizaji huyo anakabiliwa na tatizo la kamari. Georgina aidha alibainisha kwamba amekuwa akigharamia bili zote.

"Ana tatizo la kamari lakini kama kuna chochote hakukopa pesa ili kutusaidia kwa lolote, pengine kwake," ujumbe ambao Judy alidai ulitoka kwa Georgina ulisomeka.

Judy alidai kwamba watu wengine kadhaa huko Marekan pia walidai kupokea maombi sawa kutoka kwa mwigizaji huyo.

Kwenye ukurasa wa Instagram, Baha alikiri kwamba hayuko sawa na kueleza kuwa anashughulika kutatua mambo.

"Siko sawa, ninaifanyia kazi," alisema Ijumaa.

Aliendelea kufichua kuwa anauza akaunti yake ya Instagram na ya TikTok, labda ili kusuluhisha matatizo yake ya kifedha.

Aidha, imebainika kwamba muigizaji huyo na mzazi mwenzake, Georgina Njenga wameacha kufuatiliana kwenye mtandao wa Instagram, dokezo kwamba heunda mambo sio mazuri kabisa nyumbani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved