Stivo Simple Boy afunguka sababu kwa nini hajawahi kushiriki tendo la ndoa

Muhtasari

•Stivo amesema kuwa yeye ni muumini wa kweli ambaye anafuata agizo la Biblia kwamba watu hawapaswi kushiriki ngono kabla ya ndoa.

•Aidha, Simple Boy amesema anatazamia kupata takriban watoto hamsini pindi atakapojitosa kwenye ndoa.

Image: INSTAGRAM// STIVO SIMPLE BOY

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Kibra Stivo Simple Boy ameweka wazi kuwa bado hajawahi kushiriki tendo la ndoa.

Stivo amesema kuwa yeye ni muumini wa kweli ambaye anafuata agizo la Biblia kwamba watu hawapaswi kushiriki ngono kabla ya ndoa.

"Mapenzi yanafaa kufanywa kama mtu ameoa ama ameolewa. Sio mambo ya kucheza cheza hapa na pale alafu msichana akishapata mimba  jamaa anatoroka. Hiyo haifai. Sijawahi kufanya mapenzi kwa kuwa bado sijaoa," Stivo alisema katika mahojiano na Eve Mungai.

Mwanamuziki huyo alidai kuwa mahusiano yake na Pritty Vishy yalifikia kikomo baada ya mpenzi huyo wake wa zamani kutaka washiriki tendo la ndoa.

Amesema kuwa hatua yake kukataa kushiriki mapenzi haikumfurahisha kipusa huyo na ndiposa akaamua kumtema.

"Yeye hakutaka  kusikia. Alisema Simple Boy ameokoka sana ni heri aende kwa mwingine. Nilikataa," Alisema.

Simple Boy hata hivyo amesema anatazamia kupata takriban watoto hamsini pindi atakapojitosa kwenye ndoa.

Amesisisitiza kuwa watu wanafaa kuwa na watoto wengi kwa kuwa ni agizo la  Mungu wanadamu kujaza dunia.

"Inafaa watu wajaze dunia. Kiwango cha mwisho ni 30-50. Nitajaza na mpenzi wangu," Alisema.

Mwanamuziki huyo pia alisisitiza kuwa kwa sasa  hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Pritty Vishy. Alisema kwa sasa anashirikiana na mwanadada huyo katika masuala ya kikazi tu.

"Purity tunashirikiana kikazi lakini kwa mapenzi, la! Mahari tayari imeenda kwa mwingine, hivi karibuni mtamuona," Alisema Stivo.

Vishy kwa upande wake ameweka wazi kuwa hayuko tayari kurudiana na Stivo na kutangaza kuwa anatafuta mchumba mwingine.