"Tafuta Bwana Mzee mwenzio!" Harmonize amsihi Kajala huku akimvua nguo hadharani baada ya kulewa (+Screenshots)

Harmonize alisema haijulikani ni kwa nini mama huyo wa binti mmoja bado hajaolewa licha ya umri wake mkubwa.

Muhtasari

•Konde Boy kwa jeuri alimtaka Kajala kuacha kugombana naye kwenye mitandao ya kijamii na badala yake atafute mwanaume wa kumuoa.

•Kajala alikuwa amemuagiza staa huyo wa bongo fleva wakati kuweka mambo wazi wakati akilewa kama alivyokuwa ameapa.

Harmonize na Kajala
Image: INSTAGRAM//

Hatimaye,  staa wa bongo, Harmonize amejibu baada ya aliyekuwa mpenzi wake Kajala Masanja kufanya mahojiano na waandishi wa habari ambapo alijibu maswali mbalimbali kuhusu uhusiano wao uliovunjika ambao uligonga mwamba ghafla kuelekea mwishoni mwa mwaka jana.

Katika taarifa yake ndefu kwenye mtandao wa Instagram, Konde Boy kwa jeuri alimtaka muigizaji huyo mkongwe kuacha kugombana naye kwenye mitandao ya kijamii na badala yake atafute mwanaume wa kumuoa.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alidokeza kuwa haijulikani ni kwa nini mama huyo wa binti mmoja bado hajaolewa licha ya umri wake mkubwa.

“Tafuta bwana mzee mwenzio hata mganga kienyeji aliyezeeka zeheka. Acha kubishana na watoto online na kujitia moyo!! Usikute anajua anaweza kukutana na bang la take me back tena!! Kinachomfanya asiolewe hatukijuwi, kazi ni kumfwata fwata binti tuu!! Ukweli unaujua wewe!!” Harmonize alifoka siku ya Alhamisi asubuhi.

Staa huyo wa bongo aliendelea kudai kuwa Kajala amekuwa akifika kwake katika jaribio la kuomba msamaha ila walinzi wamekuwa wakimtimua.

Alimtajia muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 sehemu ya mali yake yakiwemo magari 10 na kudokeza kuwa mama yake na binti yake Zulekha Rajabu wangerithi mali yote anayomiliki iwapo angefariki leo.

“Kama unahisi sijamove on ni tatizo lako la uzee pia!! Sikukugombeza, sikukutukana. Nilikudharau na ndio maana umekuwa ukisema ukisema akimzoea mtu anamdharau. Hakuna aliyekuwa akijua hili hata watu wa karibu ndio maana kila mtu alikuwa anadhani nimecheat na sijui amelowa girl lol,” Harmonize alimwandikia ex huyo wake.

Konde Boy ziadi alimwita mpenzi huyo wake wa zamani mwizi na akamweleza bayana kuwa hafikii hata robo ya sifa za mpenzi wake wa sasa.

Mwimbaji huyo wa wimbo wa ‘Single Again’ alifoka baada ya kudokeza kuwa alikuwa amebugia tembo na kulewa. Hapo awali, alikuwa ameahidi kufunguka kuhusu uhusiano wake na Kajala uliovunjika baada ya kulewa.

“Niliwaambia nitalewa,” alisema huku akimalizia kutoa taarifa yake.

Jumatano, Kajala alipokuwa akizungumza na wanahabari alimuagiza Harmonize kujitokeza waziwazi na kuweka mambo wazi iwapo alimsaliti kimapenzi katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo walichumbiana mwaka jana.

Muigizaji huyo alitoa agizo hilo kwa Konde Boy wakati akijibu madai kuwa bosi huyo wa Konde Music Worldwide aliwahi kumfumania akimsaliti kimapenzi na mwanaume mwingine baada ya kupitia simu yake.

Kajala alimtaka staa huyo wa bongo fleva wakati kuweka mambo wazi wakati akilewa kama alivyokuwa ameapa.

“Aje aseme kama alinifumania ama nilimcheat aseme. Kama aliweza kuandika vitu vingine aseme,” Kajala alisema.

Baada ya kikao cha Kajala na wanahabari,Harmonize alidokeza amejikita katika kulewa, dokezo kuwa alikuwa tayari kuzungumza.