Tiffah amtaka Diamond atume ndege imchukue, amtafutie theluji ya kucheza nayo afikapo Tanzania

Bintiye Diamond alimtaka anunue maua, chokoleti, peremende na keki kabla ya kumchukua

Muhtasari

•Tiffah alidai kusafiri kwa ndege ya baba yake Diamond hadi Tanzania, ombi ambalo mamake alionekana kutokubaliana nalo. 

•Tiffah alisikika akijigamba kuhusu utajiri na umaarufu mkubwa wa baba yake na kumtaja Diamond  kama mtu wake wa asili.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Binti pekee wa staa wa Bongo Diamond Platnumz anayejulikana, Tiffah Dangote alishiriki katika mazungumzo na mamake Zari Hassan.

Katika mazungumzo hayo yaliyorekodiwa, Tiffah ambaye kwa sasa ana umri wa miaka sita alizungumza kuhusu maeneo mbalimbali ambayo anatazamia kutembelea mwezi huu wa Desemba hasa katika msimu wa Krismasi.

"Hatutakaa hapa. Tutaenda Brazil, tuende Cape Town alafu tuende Uganda," Tiffah alisema katika video iliyopakiwa kwenye Instagram.

Malkia huyo mdogo pia alidai kusafiri kwa ndege ya baba yake Diamond hadi Tanzania, ombi ambalo mamake alionekana kutokubaliana nalo. Zari alisisitiza kuwa anapanga kutumia likizo hiyo katika nchi ya mama yake Uganda.

Tiffah alimtaka mama yake kukatisha safari ya Uganda na hata kutishia kuchukua hatua kuhusu hilo yeye mwenyewe. Baada ya hilo aliigiza simu kwa Diamond na kumuomba atume ndege yake ili imchukue.

 "Nataka kusafiri kwa ndege hadi Tanzania. Ndege inakuja kesho?" Tiffah alisikika akisema.

Tiffah alisikika akijigamba kuhusu utajiri na umaarufu mkubwa wa baba yake na kumtaja Diamond  kama mtu wake wa asili.

Aidha, alimtaka bosi huyo wa WCB kuwa na maua, chokoleti, peremende na keki kwenye jeti kabla ya kumchukua Afrika Kusini.

"Na tutakapofika huko, je unaweza kwenda kutafuta njia ya kupata theluji? Nataka kucheza na theluji, Je! unajua kuwa napenda theluji? Ni ndoto yangu kutimia. Tafadhali, ninahitaji theluji," Tiffah alimwambia baba yake.

Binti huyo alisema kuwa vitu alivyokuwa ameviorodhesha ndivyo anavyotaka atakapofunga safari ya Tanzania hivi karibuni.

Siku ya Ijumaa, picha ya Diamond, Zari na watoto wao wawili ilichapishwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Tiffah Dangote.

"Pamoja na wazazi wangu," yalisomeka maandishi  yaliyowekwa chini ya picha hiyo nzuri ya kumbukumbu ambayo iliwaonyesha Diamond na Zari wakiwafundisha watoto hao wao kuendesha baiskeli.

Picha na ujumbe huo ziliwasisimua watumizi wengi wa Instagram wengi ambao walifurika pale kutoa maoni yao.

Chini ya chapisho hilo, jumbe  nyingi za sifa kwa wazazi hao wenza zilimiminika huku wengi wakipendekeza  kuwa wawili hao waonekana wazuri pamoja kama wanandoa. Baadhi waliwaomba warudiane.

Katika sehemu ya maoni, baadhi ya wanamitandao walionekana kutomkubali kabisa mpenzi wa sasa wa Diamond, Zuchu na kumshauri kuwa mzazi mwenzake Zari Hassan anatengeneza mpenzi bora kwake.

Siku chache Zari alishiriki mazungumzo ya simu na Mama Dangote na kumthibitishia  atakuwa nchini Tanzania katika kipindi cha  Krismasi.. Alimwambia mzazi huyo wa Diamond kwamba atawapeleka wajukuu wake Tiffah Dangote na Prince Nillan ili waweze kufurahia muda na wanafamilia wengine.