Vera Sidika afoka kwa ghadhabu baada ya mwanawe kufananishwa na ex wake, Otile Brown

Vera alitengana na Otile Brown mwaka wa 2018 baada ya kuchumbiana kwa takriban nusu mwaka.

Muhtasari

•Vera alishangaa ni kwa nini watu walimfananisha mvulana huyo wa miezi saba na mwanamume ambaye aliachana naye miaka kadhaa iliyopita.

•Nimekuwa nikipuuza hili kwa muda lakini sasa linazidi kukithiri. Wameanzisha tena na mwanangu." Vera alialamika.

 

Vera Sidika na Otile Brown wakati wa mahusiano yao
Image: HISANI

Mwanasosholaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika amejibu kwa hasira kufuatia maoni mengi ya wanamitandao waliodai kuwa mwanawe Ice Brown anafanana sana na mpenzi wake wa zamani, mwimbaji Jacob Obunga almaarufu Otile Brown

Wakati akijibu madai hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram, mama huyo wa watoto wawili alishangaa ni kwa nini watu walimfananisha mvulana huyo wa miezi saba na mwanamume ambaye aliachana naye miaka kadhaa iliyopita.

"Kwa nini mtu yeyote anadhani baba wa watoto wangu ni wa mpenzi wa zamani wa miaka iliyopita?" Vera alisema kwenye Instastori zake.

Aliongeza, "Nimekuwa nikipuuza hili kwa muda lakini sasa linazidi kukithiri. Wameanzisha tena na mwanangu.

Mrembo huyo mwenye umbo la kipekee sana aliambatanisha kauli yake na screenshots za maoni ya baadhi ya mashabiki.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mwanasosholaiti huyo kutofautiana na baba ya watoto wake, Fredrick Mutinda almaarufu Brown Mauzo baada ya kuanika uso wa mtoto wao kwenye mitandao ya kijamii bila kushauriana naye.

Muda mfupi tu baada ya mwimbaji huyo mzaliwa wa Pwani kumpost mtoto wao kwenye ukurasa wake wa Instagram, Vera pia aliweka picha za mvulana huyo wa miezi saba kwenye ukurasa wake na alionekana kumzomea kwa njia isiyo ya moja kwa moja msanii huyo ambaye amekuwa akichumbiana naye kwa takriban miaka mitatu.

"Mungu alinibariki na mtoto mzuri zaidi wa kiume @prince_icebrown. Sitaki tu furaha na afya kwa mtoto wangu, lakini pia naahidi kuwa nitatoa kila kitu ndani yangu ili kuhakikisha kuwa maisha yake yatakuwa bora zaidi. Kheri ya miezi saba @prince_icebrown.,” Vera aliandika chini ya picha yake na Ice Brown aliyoiweka.

Aliongeza, "NB: Ilibidi tu, kwani walionyesha uso bila angalau kunijulisha."

Pia aliendelea kulalamika jinsi alivyotumia pesa nyingi katika maandalizi ya kufichua uso wa mtoto wake lakini mzazi mwenzake akaharibu mipango yake,.

“Oh Wow! Hivyo ndivyo tunafanya sasa? Nilikuwa nimetumia pesa ili kupanga jambo zima. Kwa hili tu kutokea. Lo!"  aliandika.

Vera alitengana na Otile Brown mwaka wa 2018 baada ya kuchumbiana kwa takriban nusu mwaka. Wawili hao walizamia katikaa kuaibishana hadharani baada ya kuachana.