Diana akumbuka alivyotenga na mpenziwe siku alikutana na Bahati, jinsi umri ulifanya ahofie kuchumbiana naye

Diana alikutana na Bahati kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016 wakati wa kurekodi video ya wimbo wa mwimbaji huyo.

Muhtasari

•Diana alizungumza kuhusu jinsi alivyokutana na Bahati kwa mara ya kwanza wakati wa kurekodi video wa wimbo wa mwimbaji huyo.

•Licha ya awali kuwa na mashaka juu ya uhusiano wao, Diana Marua hata hivyo amebainisha kuwa anajivunia safari yao ya mapenzi.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mwanablogu Diana Marua amesimulia kwa ufupi safari yake ya mapenzi na mchumba wake Kelvin Kioko almaarufu Bahati kabla ya kuadhimisha miaka 7 ya ndoa yao.

Siku ya Jumanne, mama huyo wa watoto watatu alizungumza kuhusu jinsi alivyokutana na Bahati kwa mara ya kwanza wakati wa kurekodi video wa wimbo wa mwimbaji huyo.

Diana Marua alifichua kuwa alikuwa ameachana na mtu ambaye alikuwa akichumbiana asubuhi ya siku ambayo alikutana na Bahati kwa mara ya kwanza na akakiri kwamba hakuwa na hata mawazo ya kuingia kwenye mahusiano mengine.

"Maneno hayatoshi kuelezea jinsi Mfalme wangu ana maana kwangu. Nilipokutana na Bahati mwaka wa 2016 kama vixen/ 'bibi harusi' kwenye wimbo wake wa kwanza wa #Mapenzi, nilikuwa nimetoka tu kuachana asubuhi hiyo na hata kufikiria kuingia kwenye uhusiano basi ilikuwa ndoto,” Diana alisimulia kupitia Instagram.

Mburudishaji huyo mwenye umri wa miaka 34 aliendelea kufichua jinsi baada ya wiki chache alianza kushiriki vikao na mwanamuziki huyo wa zamani wa nyimbo za injili na kuzungumzia jinsi alivyokuwa na mashaka kuhusu kukubali kuchumbiana naye kutokana na hofu ya kuhukumiwa na jamii kutokana na tofauti zao za umri.

"Wiki chache baadaye, nilijikuta nikitembea naye na nilipenda tu vibe yake, company yake na jinsi alivyokuwa na tamaa. Hata hivyo, Kuchumbiana naye hakukuwa jambo la maana kwangu kwa sababu alikuwa ‘mdogo’ kulingana na viwango vya jamii ��� lakini kama wanasema, iliyobaki ni Historia ������,” alisema.

Licha ya awali kuwa na mashaka juu ya uhusiano wao, mama huyo wa watoto watatu hata hivyo amebainisha kuwa anajivunia safari yao ya mapenzi ya miaka saba na mafanikio waliyopata pamoja.

Mapema mwaka huu, Diana alisema kuwa alipokutana mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa mtakatifu sana, jambo ambalo hakuridhishwa nalo.

'Ulikuwa Bible, Bible, Bible, Bible. Nilikuwa nakuheshimu," Diana alimwambia Bahati wakati wa mazungumzo kwenye YouTube channel yake..

Wakati huohuo, Diana pia aliweka wazi kuwa sababu nyingine kwa nini alikuwa na shaka kuhusu kuolewa na Bahati ni tofauti zao za umri.

Alisema kwamba matarajio  yake ya awali yalikuwa kuolewa na mwanamume ambaye ni mkubwa zaidi yake kiumri.

Diana alibainisha kwamba Bahati kuwa mdogo kwake kwa miaka mitatu kulimfanya aone kana kwamba hawakufaana..

"Sababu kuu ilikuwa umri. Wewe ni mdogo kuliko mimi kwa miaka mitatu. Jamii inaamini kuwa kama mwanamke huwezi kuchumbiana na mtu mdogo kuliko yeye. Ata mimi nilijua nikitaka kutulia nitatulia na mtu ambaye ana umri mkubwa kuniliko. Bora awe mkubwa kuniliko kwa mwaka mmoja tuko sawa,” Diana Marua alimwambia mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili kwenye video hiyo.