Mtayarishaji wa maudhui wa Kenya Georgina Njenga alijibu kwa kejeli baada ya shabiki kumuuliza swali la kibishi kuhusu kupata mtoto mwingine.
Mtumiaji wa mtandao wa Instagram alimwandikia mama huyo wa binti mmoja akiuliza ni kiasi gani cha pesa ambacho angetoza kuzaa mtoto mwingine.
"Ni kiasi gani cha pesa kwa mtoto," Mtumiaji wa mtandao wa kijamii ambaye hajafichuliwa alimuuliza Georgina.
Katika majibu yake, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23 alicheka swali hilo na kudokeza kuwa hana nia ya kuzaa tena hivi karibuni.
“Heeh.. unamaanisha nini?? Mnataka kunimaliza kabisa,” Georgina alijibu.
Mtayarishaji huyo wa maudhui ni mama wa mtoto mmoja wa kike, Astra Nyambura, ambaye alizaa naye mwaka 2022. Baba wa msichana huyo mdogo mrembo ni muigizaji Tyler Mbaya almaarufu Baha ambaye Georgina sasa anashirikiana naye katika kumlea.
Mapema mwaka huu, Bi Njenga alisema katika mahojiano kuwa kwa sasa hana mpango wowote kuhusu kutafuta mtoto mwingine na kufichua kwamba kilichopo katika fikira zake na kurejelea katika kukuza maudhui muda wote.
Mama huyo wa mtoto mmoja alisema ana uhakika wa asilimia mia fil mia kwamba hatoweza tena kupata mtoto mwingine katika maisha yake, kwani ukurasa wa uzazi ndio hivyo ameshaufunga na bintiye Astra kama mtoto wa pekee.
“Kuhusu mtoto wa pili, hapana. Hapana kabisa, niko sawa. Kabisa nimeshaufunga ukurasa huo 100%,” alisema.
Kuhusu kurejea katika kukuza maudhui baada ya kupotea mitandaoni kwa muda, Georgina Njenga alisema kwamba mashabiki wake wakae mkao wa kula akidokeza huenda wakaungana na babydaddy wake kuanza kufanya video za kutoa mafunzo jinsi ya kushirikiana kulea mtoto baada ya kutengana na penzi kuvunjika.
“Sasa hivi nahisi niko sawa kwa hiyo mashabiki wangu subirini, nitakuwa naachia maudhui baada ya maudhui kwa mpigo. Labda hata tunaweza anza kuleta co-parenting content,” aliongeza.
Georgina alisema kwamba hapo awali alikuwa anatatizika kuhusu suala la kumtambulisha mtoto wake Astra katika maisha ya mitandao ya kijamii lakini kwa sasa ameshazoea jinsi utandawazi unavyoenda.