Harmonize ampongeza Diamond kwa kuiga mtindo wake wakati akichugua mpenzi mpya

Konde Boy amefurahishwa na hatua ya Diamond ya kusaka mpenzi mwenye makalio makubwa.

Muhtasari

•Harmonize anaonekana kupendezwa sana na anayedaiwa kuwa mpenzi mpya wa bosi wake wa zamani Diamond Platnumz, Fantana.

•Moja kati ya sifa za malkia huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyekulia nchini Marekani ni makalio yake makubwa.

katika siku za urafiki wao.
Harmonize na Diamond katika siku za urafiki wao.
Image: HISANI

Bosi wa Kondegang Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize anaonekana kupendezwa sana na anayedaiwa kuwa mpenzi mpya wa bosi wake wa zamani aliyegeuka kuwa hasidi wake mkuu kimuziki, Diamond Platnumz.

Hivi majuzi, kumekuwa na uvumi kwamba Diamond yuko kwenye mahusiano na mwimbaji wa Ghana, Fantana ambaye ni mshirika wake wa mapenzi katika filamu ya uhalisia cha Young, Famous and African kwenye Netflix.

Fantana ni mwimbaji na mwanamitindo wa Ghana ambaye pia ni mmoja wa wahusika wa kipindi cha ukweli cha Young, Famous and African. Hata hivyo, hana historia ya uhusiano na Diamond mbali na kuwa washiriki wa YFA2.

Moja kati ya sifa za malkia huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyekulia nchini Marekani ni makalio yake makubwa, ambayo Harmonize anaonekana kuvutiwa na kufurahishwa nayo. Alimpongeza Diamond kwa hatua hiyo.

"Karibu kwenye genge kaka, makalio," Harmonize alisema kwenye Instagram, maneno yaliyoonekana kumzungumzia Diamond.

Harmonize anafahamika kupendelea wanawake wenye makalio makubwa. Wengi wa wapenzi wake wa zamani walikuwa na sifa hiyo.

Hivi majuzi, alimtambulisha mwanasosholaiti wa Rwanda , Phiona almaarufu Yolo the Queen kama mpenzi wake mpya. 

"Sawa, siko single tena nimechukuliwa tayari," mwimbaji huyo alisema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Phiona ambaye anasemekana kuwa mmoja wa wanasosholaiti waliofanikiwa zaidi nchini Rwanda na viunga vyake ameweza kuvutia hisia za watumiaji wengi wa mitandao kutokana na umbo maalum wa mwili wake.

Mwanadada huyo mrembo amebarikiwa kuwa na mwili uliopinda na makalio makubwa ambayo wanaume wengi wanayatamani. Anajulikana zaidi kwa misemo yake ya kuvutia 'Wake Pray Slay' na 'Tamu kuliko asali.'

Harmonize alimtambulisha kama mpenzi wake mpya takriban miezi mitano baada ya kutengana na muigizaji Kajala Masanja ambaye pia ana makalio makubwa na kiuno kilichochongwa vizuri na Muumba.

Ni tabia ya Harmonize kuchumbiana na wanawake wenye makalio makubwa, na anaonekana kufurahishwa na Diamond kufuata nyayo zake.