Msanii wa bongo Mbosso ni msanii kutoka Tanzania ambaye amekuwa akitia bidii kila siku katika kazi yake ya usanii.
Siku mbili zilizopita msanii huyo alitoka kibao akimshirikisha msanii wa Uganda Spice Diana, kibao ambacho kinafahamika kama 'Yes'.
Ni kibao ambacho kimepokelewa vyema na mashabiki kinazungumzia mwanamume ambaye alikuwa anatafuta mpenzi na hatimaye amempata mpenzi wa roho yake.
Huku akimuuliza kama atakubali amuoe, na bila shaka mwanamke huyo anakubali, na hata kumpeleka kwa wazazi wake.
Furahia kibao hicho cha wiki, na utoe maoni yako kama kina weza au bado.
Hii hapa video ya kibao hicho;