Fikra za Bahati

Je, Bahati ameacha injili? Tazama kibao chake kipya

Kwenye kibao hicho, Bahati amesikika akiwadhalilisha wasanii wengine kama Sauti Saul, Ringtone, Khaligraph na Octopizzo.. Khaligraph amjibu

Muhtasari

•"Alafu naskia Bahati ameanza bangi na sigara ameanza kurap matusi, punguza iyo bangi baba wacha kiherehere" Khaligraph alimjibu Bahati.

•Kwenye video hiyo, Bahati pia anaonekana kwenye klabu akivuta sigara kubwa

Bahati
Bahati
Image: Hisani

Mwanamuziki wa nyimbo za injili  na mapenzi Kelvin Kioko ameachilia kibao kipya kwa jina 'Fikra za Bahati' kwenye mtandao wa Youtube.

Title : Fikra Za Bahati Artist : Bahati Album : Love Like This #Bahati #LoveLikeThisAlbum

Kwenye kibao hicho, Bahati amesikika akiwadhalilisha wasanii wengine kama Sauti Saul, Khaligraph na Octopizzo.

Picha za video hiyo zilizokuwa zimeonyeshwa kabla ya video kuachiliwa na ambazo zilionyesha Bahati akivuta sigara kubwa zilikuwa zimeibua hisia mbalimbali miongoni mwa Wakenya huku ikisemekana kuwa huenda msanii huyo ameiaga injili.

Ringtone ni mmoja wa wasanii waliomkahifu Bahati huku akisema kuwa Bahati alikuwa ameacha injili na kuingilia utumizi wa madawa ya kulevya.

 

Khaligraph ambaye kwa sasa ako katika ziara nchini Marekani amemjibu Bahati huku akimwambia awache bangi na apunguze Kiherehere.

"Alafu naskia Bahati ameanza bangi na sigara ameanza kurap matusi, punguza iyo bangi baba wacha kiherehere" Khaligraph alimjibu Bahati.

Bahati amesema kuwa kibao hicho ni cha kuwatayarisha mashabiki wake kwa albamu yake 'Love like this' ambayo ataachilia hivi karibuni.