(+Video) Bahati awachilia kibao cha pili kwenye albamu yake 'Love like this'

Ameweza, Hajaweza?

Muhtasari

•Mapema wiki iliyopita aliwachilia kibao 'Pete Yangu' ambacho alishirikisha Nadia Mukami na kimeendelea kupokelewa vizuri sana huku kikiandikisha zaidi ya watu 1.3M ambao wametazama ndani ya kipindi cha wiki moja tu,

Bahati
Bahati
Image: Instagram

Baada ya kuzindua albamu yake Jumapili ya tarehe 13 mwezi Juni, mwanamuziki wa nyimbo za injili na za mapenzi Kevin Bahati almaarufu kama 'mtoto wa mama' anawachilia kibao kimoja kimoja kutoka kwenye albamu hiyo.

Mapema wiki iliyopita aliwachilia kibao 'Pete Yangu' ambacho alishirikisha Nadia Mukami na kimeendelea kupokelewa vizuri sana huku kikiandikisha zaidi ya watu 1.3M ambao wametazama ndani ya kipindi cha wiki moja tu,

Baada ya wiki moja amewachilia kibao cha pili "Take it slow" (ipeleke kwa mwendo wa pole pole) ambacho hajashirikisha yeyote.

Wimbo huo ni wa mapenzi. Utazame hapa.

STREAM THE ALBUM EXCLUSIVELY ON BOOMPLAY LINK BELOW http://Boom.lnk.to/BahatiLoveLikeThisAlbum Title: Take it Slow Artist : Bahati Album : LOVE LIKE THIS Audio : Mesesi & Teddy B #Bahati #LoveLikeThis #TakeItSlow

Je ameweza, hajaweza?