WAMEWEZA, HAWAJAWEZA?

(+Video) +254 yapatana na Bongo: Mastaa Otile Brown na Darassa watoka jikoni na kibao moto

Baada ya kuwa jikoni kwa muda hatimaye Otile Brown na staa wa Bongo Darassa wametupakulia kibao moto kweli.

Muhtasari

•Baada ya kuwa jikoni kwa muda hatimaye Otile Brown na staa wa Bongo Darassa wametupakulia kibao moto kweli.

•Hapo awali Otile alikuwa amedai kuwa kulikuwa na vikwazo vilivyofanya kibao hicho kisiachiliwe wiki iliyopita ila kwa sasa wimbo huo unapatikana YouTube.

Image: INSTAGRAM// OTILE BROWN

Baada ya kuwa jikoni kwa muda hatimaye Otile Brown na staa wa Bongo Darassa wametupakulia kibao moto kweli.

Wawili hao ambao wana weledi mkubwa wa mistari ya muziki na ufuasi mkubwa kote Afrika Mashariki wameshirikiana kuimba kibao 'K.O(Tiktok)' ambacho kimepakiwa mtandaoni wa YouTube alasiri ya leo.

Wimbo huo ambao ni wa kusifia urembo wa wanadada unaanza na sehemu ya Otile Brown kisha kufunga na sehemu ya Darassa.

Hapo awali Otile alikuwa amedai kuwa kulikuwa na vikwazo vilivyofanya kibao hicho kisiachiliwe wiki iliyopita ila kwa sasa wimbo huo unapatikana YouTube.

"Nafahamu tulistahili kuachia wimbo wiki hii ila kuna mambo hayajakuwa sawa.,. na kwa kuwa wiki tayari imeisha tunaomba tutoe wiki ijayo" Otile alisema Ijumaa wiki iliyopita.

Tazama:-

#OtileBrown #Darassa # K.O #NgommaKenyanMusic Just In Love Music presents the official music video for #Knockout performed by Otile Brown X Darassa. The audio is produced, Mixed and Mastered by Vicky Pondis Video shot and Directed by Hanscana. Connect with Otile Brown on Social Media: For More Information on Booking: Phone number: +254799764477 Email: noriegareginald@gmail.com ©2021 Just In Love Music Limited.All rights reserved

Je maoni yako ni yepi kuhusiana na kibao 'K.O' wameweza au la??

Wimbo huo umepokewa vyema na mashabiki huku ukiwa umetazamwa na zaidi ya watu 30,000 tangu kuachiliwa.