Diamond azindua ngoma mpya - Naanzaje

Muhtasari

• Sawa na ngoma zingine za Diamond kibao Naanzaje ni cha mapenzi. 

Image: WASAFI

Staa wa bongo Diamond Platnumz amezindua kibao moto toka jikoni 'Naanzaje'.

Siku moja tu baada ya kupakiwa kwenye Youtube kibao hicho kilikuwa tayari kimeanza kutikisa anga za wapenzi wa bongo.

Sawa na ngoma zingine za Diamond kibao Naanzaje ni cha mapenzi. 

Staa mwenza wa bongo Rayvanny kupitia mtandao wa Twitter aliwajulisha mashabiki wake kuhusu ngoma mpya ya Diamond.