Usitumie jina langu kutafuta kiki,'Eric Omondi amshambulia msanii Prezzo

Muhtasari
  • Wikendi iliyopita Prezzo alimshambulia Eric, na kumshauri aamue kitu kile anataka maishani mwake na wala sio kuwa amechanganyikiwa

Kwa muda sasa mchekeshaji Eric Omondi amekuwa akivuma mitandaoni baada ya kuwaambia wasanii wa kenya waamke, na kudai kwamba tasnia hiyo imekufa kwa muda.

Wikendi iliyopita Prezzo alimshambulia Eric, na kumshauri aamue kitu kile anataka maishani mwake na wala sio kuwa amechanganyikiwa.

Akitumia ukurasa wake wa Instagram Prezzo aliandika,

"Vazi nzuri ndugu yangu lakini fanya uamuzi. Ni Jimmy Wanjigi," ni mke au kiki??? @ericomondi 🤔 Usitafune zaidi ya unavyoweza kumeza." Aliandika Prezzo.

Je, Eric alisikiliza ujumbe huo? Hapana! Kwa kweli, aliendelea kujibu maandishi ya rappa huyo.

"USITUMIE JINA LANGU Kwa kiki yenye bei nafuu😡😡😡. Kwanza kabisa, VAZI hili ni la 473K. PILI SASA HIVI NILICHOLENGWA NA KUHUSU KIWANDA CHAKO KILICHOFARIKI na CHACHE UNAchoweza kufanya ni kushukuru na KUWEKA Baadhi. Heshimu JINA langu." ERic alimjibu Prezzo.

Wasanii tofauti nchini wametoa maoni yao kuhusu mjadala wake Eric Omondi na asilimia kubwa wanaonekana kupinga wazo lake.