logo

NOW ON AIR

Listen in Live

LOUI amshirikisha msanii Kidi na Maud Elka kwenye kibao chake cha Hennessy

Pia aliwashukuru wasanii hao wawili kwa kujitolea kwao, na kwa msaada wao.

image
na Radio Jambo

Burudani06 July 2022 - 13:30

Muhtasari


  • Loui amshirikisha msanii Kidi na Maud Elka kwenye kibao chake cha Hennessy

Miezi chache baada ya kuwa nambari nne, kwa wafuasi wanaosikizwa kwenye spotify nchini Tanzani msanii Loui amemshirikisha msanii kutoka Ghana Kidi na  Maud Elka kwenye kibao chake cha Hennessy.

Wasanii wengine walioongoza katika kuwa na wafuasi wengi kwenye spotify ni pamoja na staa wa bongo Diamond Platnumz,Rayvanny na Harmonize.

Msanii Kidi alifahamika sana kupitia kwenye kibao chake cha 'touch it'.

Kushirikishwa kwake Hidi na Maud kwenye kibao hicho kunaleta mdundo mwingine unaowawezesha mashabiki wake kufurahia kibao hicho.

Kibao chake Loui kimezalishwa na S2kizzy, huku video yake ikiwa imefanyika Tanzania Dar Es Salaam, na kuelekezwa na Director Kenny.

Huku akizungumzia kibao hicho Loui alisema kwamba ni mradi ambao alikuwa ameusuburi kwa muda.

Pia aliwashukuru wasanii hao wawili kwa kujitolea kwao, na kwa msaada wao.

"Nimekuwa nikitarajia toleo hili kwa furaha msisimko, sote tumeweka kazi nyingi, wakati, na bidii katika mradi huu na natumai utakupa kila sababu ya kufurahia na kucheza tena wimbo huu katika msimu wa kiangazi. Nampongeza KIDI na Maud Elka kwa msaada wao juu ya hili, mradi huu haungewezekana bila ubunifu wao mchango na kujitolea”.

Hii hapa video ya kibao hicho;

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved