logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mama wavulana! Njugush na Wakavinye hatimaye wafichua kuzaliwa kwa mwanao wa pili

Bi Ndinda alifichua kuwa mwanao Toria alizaliwa mwezi mmoja uliopita.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri17 September 2022 - 08:50

Muhtasari


•Wanandoa hao walikuwa wameziweka siri habari kuhusu mtoto wao tangu kuzaliwa kwake mwezi uliopita.

Wanandoa mashuhuri Blessed Njugush na Celestine Ndinda wametangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bi Ndinda alifichua kuwa mwanao Toria alizaliwa mwezi mmoja uliopita.

"Ni mwezi mmoja sasa tangu tulipokaribisha mwanachama mpya wa familia yetu, Baby Toria. Shukran kwa maombi na jumbe za kheri njema," alitangaza siku ya Jumamosi.

Aliongeza "Mama Boys, Tugi & Toria (inyaa tuvisi)."

Wanandoa hao walikuwa wameziweka siri habari kuhusu mtoto wao tangu kuzaliwa kwake mwezi uliopita.

Wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri walifurika chini ya ujumbe huo kuwapongeza  kwa zawadi ya mtoto.

Kabiwajesus Hongera 😍

Bettymuteikyallo Hongera Ndinda. Familia yako ibarikiwe. Najua Tugi amefurahi! Muwe sawa.❤

Kalekyemumo Awww Hongera inyaa tuvisi 🥳🥳🥳🥳

Milly Chebby Hongera Mama Boys

giladmillo ❤❤❤

Habari kuhusu ujauzito wa pili wa BiNdinda na mumewe  Njugush zilikuja kufichuka takriban miezi mitano iliyopita wakati wa tamasha lao la TTT3 ambalo waliandaa katika ukumbi wa Nairobi Cinema. 

Wanandoa hao ambao pia ni waigizaji wenza wamekuwa katika ndoa kwa takriban miaka sita na tayari wana mtoto mwingine mmoja wa kiume pamoja, Tugi ambaye alizaliwa  mnamo mwezi Machi, 2018.

Wawili hao walifunga pingu za maisha mwezi Desemba 2016 na wakagundua ujauzito wa mtoto wao wa kwanza rtakriban miezi  minne baadae.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved