Nadia Mukami msanii wa kwanza wa kike kufikisha 'streams' milioni 10 kwenye Boomplay

Muhtasari
  • Nadia Mukami msanii wa kwanza wa kike kufikisha 'streams'milioni 10 kwenye Boomplay
Nadia-2-e1566897594626-696x395
Nadia-2-e1566897594626-696x395

Mwimbaji wa kike wa Kenya na mtunzi wa nyimbo Nadia Mukami amekuwa akifanya harakati kubwa katika tasnia ya muziki na bado anafanya hivyo.

Msanii huyo ametambuliwa kama msanii wa kwanza wa kike nchini Kenya kufikisha 'streams' milioni 10 kwenye muziki wa Boomplay.

Nadia kupotia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwashukuru mashabiki kwa kuwa naye kila wakati na pia kutazama muziki wake.

Wakati huu wa janga la corona wasanii wengi walionekana kufifia katika kazi yao ya usanii, lakin Nadia alitia bidii na kutoa kiao kimoja baada ya kingine.

"Milioni kumi asanteni sana timu Nadia,nimebarikiwa kuwa nanyi, nadhani sasa tunahitaji kibao kipya," Alishukuru Nadia.

Hizi hapa jumbe za mashabiki;

mac_wangari: ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘ wow great job girl๐Ÿ˜Š

dahuu_mkenya: Congratulations popstarโค๏ธ

silaw_sang: congratulations kanadia kangu๐Ÿ˜๐Ÿ˜katambe tu๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

lilpop965: ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ u should upload another ๐Ÿ˜๐Ÿ˜

jadabra_cleaning_fumigation: Congratulations ma'am

Pia Boomplay iliweka wazi kwamba Nadia ni msanii wa nne nchini Kenya kufikisha watazamaji hao