'Niwakati wako wakuwashukuru walio kukatisha tamaa,'Harmonize ampongeza msanii Ibraah

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alimshauri Ibraah atie bidii, na kwamba ni wakati wake wa kuwashukuru wote waliomkatiza tamaa ya usanii
  • Pia alimpongeza msanii huyo kwa bidii yake

Msanii wa bongo kutoka Tanzania Harmonize amempongeza,msanii mwenake ambaye amemsajili kwenye ebo ya Ibraah baada ya kibao chake kupokea watazamaji milioni 1 kwa muda wa masaa15.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alimshauri Ibraah atie bidii, na kwamba ni wakati wake wa kuwashukuru wote waliomkatiza tamaa ya usanii.

Pia alimpongeza msanii huyo kwa bidii yake.

"HONGERA NDUGU YANGU @ibraah_tz 🤴 NI WAKATI WAKO SASA KUWASHUKURU WOTE WALIOKUKATISHAGA TAMAA ...!!! NA KUKUMBUKA YALE MAGUMU ULIYOYAPITIA NA KUYAHESABU KAMA ZILIKUWA CHANGAMOTO ILII UUONE UKUU WA MUNGU ...!!!! GO GO GO ...!!!! KEEP GOING AND MAKE THE TEAM PROUD (1.m) B4 THE DAY #KONDEGANG4YOU RUN IT UP MY PEOPLE @ibraah_tz 🦅🦅🦅🦅🦅🦅🦅,"Aliandika Harmonize.

Kibao chake Ibraah cha 'Jipinde' kilipokea watazamaji milioni moja kwenye youtube kwa muda wa chini wa masaa kumi.

Baadhi ya wanamitandao walimpongeza, ilhai wengine walisema kwamba Harmonize na timu yake walikuwa wamenunua maoni na watazamaji kwenye youtube.