'Nataka kumuomba msamaha,'Bien amuomba Khaligraph Jones msamaha huku akifichua wanatoa EP pamoja

Muhtasari
  • Bien amuomba Khaligraph Jones msamaha huku akifichua wanatoa EP pamoja
  • Msanii huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, amefichua kwamba Jones alimuomba msamaha
  • Awali wawili hao walishirikiana na kutoa collabo pamoja kabla ya mambo hayajageuka na kueneza chuki
Bien na Khaligraph Jones
Image: Bien/INSTAGRAM

Bien amefichua kuwa yeye na Khaligraph Jones wanafanyakazi pamoja kwa ajili ya EP ambayo anatarajia kutoa.

Pia Bien pia aliomba msamaha kwa Papa Jones baada ya kumkejeli kwa ajili ya mwili wake, na kumuita mtoto kwa miaka 4.

Msanii huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, amefichua kwamba Jones alimuomba msamaha.

Awali wawili hao walishirikiana na kutoa collabo pamoja kabla ya mambo hayajageuka na kueneza chuki.

"2022 ilianza kwa kasi!Adui wangu wa muda mrefu @khaligraph_jones aliniomba msamaha na akakiri kuwa nilikuwa sahihi wakati wote (hawezi kupata abs ikiwa atanyanyua vyuma kwenye mazoezi tu).

Kwa hivyo sasa ni wajibu wangu kumsaidia kubadili mlo wake na kudhibiti utaratibu maalum wa mazoezi uliobuniwa kuhusu utimamu wa mwili badala ya kujenga mwili.

2022 tunafanya OG aonekane mzuri tena kwa sababu amerudi kwenye orodha yangu ya rappa bora na ni wapendao Afrkana wakati  tunafanya EP nzima pamoja, atakuwa anaheshimika duniani kote.

Pia nataka kuchukua nafasi hii nzuri kumuomba radhi kwa kumuita mnene kwa miaka mitatu mfululizo, hapana ngoja, nadhani ni miaka minne kweli. Ni vile saa hii sina simu, ningeweza kumpigia simu ana kwa ana lakini chapisho litafanya kwa sasa," Bien amesema.