logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond amenishindia followers na uchawi,'Ringtone ajigamba

"Kitu pekee ambacho Diamond ananishinda ni wafuasi na uchawi tu.

image
na Radio Jambo

Burudani14 January 2022 - 09:32

Muhtasari


  • Msanii Ringtone ajigamba kwamba amemshinda Diamond kwa utajiri

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko, kwa muda sasa amekuwa akijigamba na kusema kwamba ndiye msanii tairi zaidi Afrika Kusini.

Akizungumza na Mpasho Rigntone alidai kwamba kitu ambacho staa wa Bongo Diamond Platnumz amemshinda nacho ni kuwa na wafuasi wengi mitandaoni na uchawi.

"Kitu pekee ambacho Diamond ananishinda ni wafuasi na uchawi tu. Linapokuja suala la pesa na maisha makubwa mimi niko mbele yake sana. Mwambie anifanyie uchunguzi. Pesa ya Kenya ina nguvu kuliko fedha ya Tanzania," Ringtone Alizungumza.

Huku akizungumzia siasa alisema kuwa;

"Nina marafiki zaidi ya 20 ambao ni  wanasiasa lakini nina ushawishi zaidi kuliko wao. Nilidhani kwa kujiunga na siasa unakuwa na ushawishi zaidi lakini sivyo.

Eric Omondi ana nguvu zaidi kwa sababu ana sauti kubwa zaidi, Sauti Sol nawapenda pia lakini nachukia jinsi wanavyopenda wanawake wanaochumbia. Lakini ushawishi walio nao ni mkubwa sana ikilinganishwa na kama wangekuwa kwenye siasa."

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved