Diana Marua akaribia kukomboa akaunti yake ya Youtube

Muhtasari

• Msanii chipukizi Diana Marua amesema kwamba hatua ya kumtambua aliyeidukua akaunti yake ya Youtube inaendelea kutoa matumaini.

• Marua alisema kwamba mchakato wa kuhakikisha akaunti hiyo imerejea katika jina lake inaendelea na anaamini atarejelea kazi yake Kama kawaida.

• Pia ameshukuru usimamizi wa YouTube na kampuni ya NGOMMA kwa kuingilia kati swala hili na pia mashabiki wake kwa kumtilia dua.

Diana Marua
Diana Marua
Image: hisani

Msanii chipukia Diana Marua amesema kwamba hatua ya kumtambua aliyeidukua akaunti yake ya Youtube inaendelea kumpa matumaini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema kwamba mdukuzi huyo aliyebadilisha jina la akaunti kuwa Ark Invest, alifuta video kadhaa na kubadilisha jina la akaunti hiyo na baadaye kuchapisha kazi ambazo zinakwenda kinyume na sheria za kampuni ya Youtube, Jambo lililopelekea akaunti hiyo kufungwa.

Marua alisema kwamba mchakato wa kuhakikisha akaunti hiyo imerejea katika jina lake inaendelea na anaamini atarejelea kazi yake Kama kawaida.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

"Some good news! My YouTube channel is almost back. Unfortunately, the hacker had deleted several videos and changed the name to Ark Invest which used my channel to post content that violates YouTube guidelines and immediately i was flagged off as a user," alisema Marua.

Pia ameshukuru usimamizi wa YouTube na kampuni ya NGOMMA kwa kuingilia kati swala hili na mashabiki wake kwa dua zao.

Diana Marua pia amewasihi mashabiki zake kuwa watulivu huku wakishughulikia swala hilo na kurejelea hali ya kawaida ya kuwaburudisha kupitia kazi zake.