Imetosha! Uwoya avunja kimya kuhusu sakata la Aristote na Sepetu.

Muhtasari

• Muigizaji na mfanyibiashara, Irene Uwoya Jumatatu ya tarehe 31/01/2022 amepelekea kwenye ukurasa wake wa Instagram kuomba msamaha kwake Wema Sepetu kutokana na maneno ya kuchukiza aliyoyasema rafiki yake Aristote.

• Aidha ameongeza kuwa amempigia simu Aristotee na kuonyesha kutofurahishwa kwake kwa kitendo hicho alichokifanya ambacho kinaonekana kuleta uchonganishi kati yao.

Irene Uwoya
Image: Ireneuwoya/INSTAGRAM

Muigizaji na mfanyibiashara, Irene Uwoya Jumatatu ya tarehe 31/01/2022 amepelekea kwenye ukurasa wake wa Instagram kuomba msamaha kwake Wema Sepetu kutokana na maneno ya kuchukiza aliyoyasema rafiki yake Aristote.

Uwoya anasema kwamba anajutia sana maneno hayo yasiyo ya kibinadamu yaliyozungumzwa na rafiki yake huyo, na kusisitiza kwamba hajawahi kumtuma Aristote kuzungumza maneno ya kuchafua roho kuhusu waigizaji wenzake, jambo ambalo linazidi kuzua chuki miongoni mwao kila uchao.

 Sijawahi kumtuma Aristote amtukane Wema wala mtu yeyote yule, sina ugomvi na Wema na sina sababu ya kufanya upuuzi wa namna hiyo, Nimempigia pia Aristote kuoneshwa kukasirishwa kwangu, na niseme tu hiyo ni MIHEMKO yake yeye, sihusiki na lolote juu ya hayo aliyoyaropoka ambayo yanaleta hata uchonganishi baina yetu kitu ambacho sikifurahii kwakweli,” aliandika Uwoya.

Aidha ameongeza kuwa amempigia simu Aristotee na kuonyesha kutofurahishwa kwake kwa kitendo hicho alichokifanya ambacho kinaonekana kuleta uchonganishi kati yao, na kuweka wazi kwamba hajawahi kuwa na mvutano wowote na Wema Sepetu.

Amesema kwamba anathamini upendo wa Aristote kwake ila angefurahi zaidi iwapo mapenzi hayo yangesalia kati yao bila kumlinganisha na watu wengine.  “ Ningeheshimu sana kama itabaki sisi na maisha yetu bila kulinganisha wala kunishindanisha na yeyote yule sababu mimi naishi maisha yangu siko kwenye mashindano na mtu, asanteni wote,one love,” aliongeza Uwoya.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya Aristote kupitia mahojiano na kituo kimoja cha habari, kutoa kauli iliyoonekana kumlinganisha Uwoya na Sepetu kwa misingi ya mali wanayomiliki jambo lililopelekea Sepetu kugadhabika na kumskashifu vikali Aristote.

Sasa kinachosubiriwa ni kuona iwapo Wema Sepetu atakubali samahani hiyo na kuzika maneno ya Aristote katika kaburi la sahau.