Tumeanza vikao, Nandy Festival ya 2022 mtaipenda- Nandy

Muhtasari

• Msanii wa kike kutoka Tanzania, Nandy amesema kwamba tamasha lake la Nandy Festival linarejea hivi karibuni.

• Tamasha hilo mwaka jana lilifanyika katika mikoa mbalimbali huku mashabiki wakijitokeza kwa wingi kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii waliopata nafasi kuingia jukwaani.

The Africa princess 'Nandy'
The Africa princess 'Nandy'
Image: Facebook/ Nandy

Msanii wa kike kutoka Tanzania, Nandy amesema kwamba tamasha lake la Nandy Festival linarejea hivi karibuni.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Nandy amesema kwamba vikao vya kupanga mikakati ya tamasha hilo mwaka huu wa 2022 tayari vishaanza huku akiwaomba mashabiki kuwa ange kusapoti  shughuli hiyo.

“Kikao cha kwanza cha leo cha mwaka huu cha Nandy Festival 2022. Mshindwe nyie mashabiki!!!” aliandika Nandy.

Tamasha hilo mwaka jana lilifanyika katika mikoa mbalimbali huku mashabiki wakijitokeza kwa wingi kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii waliopata nafasi kuingia jukwaani.

Kikubwa kinachosubiriwa ni kuona utofauti gani ambao Nandy ataleta katika tamasha hili kuanzia kwa muundo wa jukwaa, wasanii atakaowaleta na hata pia mbinu yake ya kufanya mauzo ya tamasha hilo.

Kwingineko, baadhi ya mashabiki wanazidi kushangaa iwapo Nandy ataweza kurudia miondoko yake ya densi aliyotumia mwaka jana ikifahamika kwamba mwanadada huyo ameongeza uzani  si haba. Baadhi ya ‘comment’ zilisoma: “Awee ilikua pambe, sasa hivi utaweza au twende gym kwanza.”

Nandy ambaye siku chache zilizopita  amesherehekea ngoma yake ya Nimekuzoea kutazamwa na watu milioni kumi, anakuwa miongoni mwa wasanii wa kike ambao wanafanya kazi ya kupigiwa mfano ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

La mno kwa sasa ni kusubiria taarifa rasmi kutoka kwake Nandy kufahamu tamasha hilo linaanza rasmi lini na mashabiki wajiandae kwa burudani la aina gani.