logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tarehe 10/02/2022, tetemeko la EP yake Rayvanny.

Msanii kutoka bongo, Rayvanny almaarufu Chui amesema kwamba anakwenda kuachia EP yake ya kwanza ya 2022 mnamo tarehe 10/02/2022.

image
na Davis Ojiambo

Burudani01 February 2022 - 08:04

Muhtasari


  • • Msanii kutoka bongo, Rayvanny almaarufu Chui amesema kwamba anakwenda kuachia EP yake ya kwanza ya 2022 mnamo tarehe 10/02/2022.
  • • Miongoni mwa wasanii watakaofankiwa kuingia katika EP hiyo ni pamoja na: Nadia Mukami, Guchi, Ray C, Marioo, Clyde, Roki pamoja na Zuchu.
  •  
Rayvanny

Msanii kutoka bongo, Rayvanny almaarufu Chui amesema kwamba anakwenda kuachia EP yake ya kwanza ya 2022 mnamo tarehe 10/02/2022.

Kulingana na picha ambayo ameachia kwenye ukurasa wake wa Instagram, EP hiyo yenye title ya FLOWERS II itakuwa na ngoma tisa huku ikishuhudia kolabo na wasanii tofauti ndani ya Tanzania na mataifa mengine ya nje.

Miongoni mwa wasanii watakaofankiwa kuingia katika EP hiyo ni pamoja na: Nadia Mukami, Guchi, Ray C, Marioo, Clyde, Roki pamoja na Zuchu.

‘Post hii inajiri siku chache tu baada ya ngoma yake ya #mamtetema aliyomshirikisha msanii Maluma kutoka Colombia kufanya vizuri katika chati tofauti za taifa la Mexico.

Kulingana na wasanii ambao wamehusishwa humo, sni bayana kwamba itakuwa EP ambayo itatetemesha mawimbi ya burudani ndani ya Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki kwa ujumla.

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved