Azziad azungumzia kukejeliwa mitandaoni baada ya umaarufu

Muhtasari

• Mwanamitindo Azziad Nasenya amezungumza jinsi alivyokejeliwa na kudhalilishwa mitandaoni pindi tu alipopata umaarufu mapema mwaka 2020.

• Nasenya alipata umaarufu baada ya mkanda wa video akicheza densi ya kibao ambacho msanii Femi One alimshirikisha Mejja, almaarufu Utawezana kusambazwa mitandaoni kwa wingi mno.

Azziad Nasenya
Image: Facebook

Mwanamitindo Azziad Nasenya amezungumza jinsi alivyokejeliwa na kudhalilishwa mitandaoni pindi tu alipopata umaarufu mapema mwaka 2020.

Nasenya alipata umaarufu baada ya mkanda wa video akicheza densi ya kibao ambacho msanii Femi One alimshirikisha Mejja, almaarufu Utawezana kusambaa mitandaoni kwa wingi mno.

Mwanamitindo huyo ambaye anajulikana pakubwa kwa kuunda video fupi akicheza densi na kisha kuzitundika katika mtandao wa TikTok anasema alidhalilishwa sana mitandaoni kwa miezi mitatu mpaka kidogo aathirike kwa unyongovu.

“Ilikuwa ngumu mwanzoni, kwa watu kunikejeli mitandaoni. Nilikaribia kuathirika kwa unyongovu lakini kwa bahati nzuri nilikuwa karibu na watu walionijali na kunipenda na walinisaidia sana kushinda majaribu hayo,” alisema Nasenya katika hafla moja alipokuwa akizinduliwa kama balozi wa kampuni ya Bic Februari 1.

Nyota huyo wa TikTok anasema kuwa kwa sasa ashajua tabia ya watu wa mitandaoni na hata hashughuliki nao vile.

“Mwisho wa siku najua pia kwamba Yesu alidhalilishwa na kukejeliwa na kwa maana hiyo mimi siwezi tegemea kwamba nitakuwa mkamilifu. Si kila mtu ambaye atapenda kile unachofanya na vilevile si kila mtu ambaye atachukia kile unachofanya,” alisema Nasenya.

Nasenya alizinduliwa kama balozi wa Bic Jumanne Februari 1