Miss P ni msanii mzuri lakini hajitumi - Erick Omondi

Muhtasari

• Mcheshi Erick Omondi hatimaye amejitokeza na  kujibu madai ya msanii Miss P akisema kwamba yeye na usimamizi wake [Big Time Entertainment] walitimiza jukumu lao  la kumrejesha mwanamuziki huyo kwenye burudani.

• Omondi amekiri kwamba lebo yake haina uwezo wa kuwasajili wasanii chini ya mkataba ila wanaweza tu kumpa sapoti msanii kufika kiwango anachotaka yeyey halafu wanamuachilia ili aendelee na kazi zake.

Erick Omondi
Erick Omondi
Image: Instagram KWA HISANI

Mcheshi Erick Omondi hatimaye amejitokeza na  kujibu madai ya msanii Miss P akisema kwamba yeye na usimamizi wake [Big Time Entertainment] walitimiza jukumu lao  la kumrejesha mwanamuziki huyo kwenye burudani kwa kile alichokitaja kwamba alikuwa amezama baada ya kuende njia panda na usimamizi wa Saldido International ambayo ilikuwa lebo yake Willy Paul.

Omondi amekiri kwamba lebo yake haina uwezo wa kuwasajili wasanii chini ya mkataba ila wanaweza tu kumpa sapoti msanii kufika kiwango anachotaka yeyey halafu wanamuachilia ili aendelee na kazi zake.

Hata hivyo mcheshi huyo amaarufu rais wa ucheshi Afrika ameweka wazi kwamba kwa kipindi ambacho alifanya kazi na Miss P, alitumia kiasi kikubwa cha pesa jambo ambalo usimamizi wake haukukubaliana nalo. Ameongeza kuwa walikuwa wamepanga kazi zingine na wasanii wakubwa kama vile Bien wa Sautisol na Harmonize kutoka Tanzania.

Aidha Omondi amesema kwamba usimamizi wa Bigtime Entertainment haukuona uwezekano wao kutengeneza kipato kutoka kwa msanii huyo na hivyo kukosa kumsajili huku wakidai kwamba Erick Omondi alikuwa ametumia hela nyingi kwake ila hawakuona faida na wala hawakuelewa mikakati na mipango yake ilikuwa ipi kwa msanii huyo.

Kwa upande wake Omondi amejitetea kwa kutochukua simu za Miss P kwa kie alichosema kuwa alikuwa akipata meseji zisizoeleweka kutoka kwa msanii huyo kupitia Instagram ila baadaye aligundua kwamba akaunti ya Instagram ya msani huyo ilikuwa imedukuliwa.

Vilevile ametoboa siri kwamba alikuwa amezungumza pembeni na aliyetarajiwa kuwa meneja wa Miss P, Jimmy kwamba angekata mawasiliano na binti huyo ili kwamba aweze kutangamana na kujenga uhusiano mzuri na usimamizi wake ambao Omondi alikuwa amemkabidhi kwao ili waweze kufanya kazi kwa njia safi.

Omondi amesema kwamba anaaminia sana kipaji chake Miss P na angependa kumuona akitamba katika sekta ya burudani. Kwa sasa mashabiki wanasubiri kuona iwapo wawili hao watakutana na kusuluhisha tofauti zao na msanii huyo ataweka mikakati gani kujisukuma mbele.