Willy Paul amhongera Queen P baada ya ngoma kutinga views milioni moja

Muhtasari

• Msanii Willy Paul amempongeza mwanamuziki Miss P , hii ni baada ya ngoma yake #Pressure kutinga views milioni moja kwenye mtandao wa Youtube.

• Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa ameambatanisha na picha ya Miss P, Pozze amemhongera kwa kuwahi views milioni moja kwa ngoma yake ya kwanza chini ya usimamizi wa Saldido International Records.

W.I.L.L.Y P.O.Z.Z.E
W.I.L.L.Y P.O.Z.Z.E
Image: Instagram KWA HISANI
W.I.L.L.Y P.O.Z.Z.E
W.I.L.L.Y P.O.Z.Z.E
Image: Instagram KWA HISANI

Ifahamike kwamba huyu ni  msanii wa pili wa kike chini ya lebo yake Willy Paul baada ya kuondoka kwa Miss P ambaye pia waliachia kazi kadhaa na Pozze ila baadaye uhusiano wao ukasambaratikakwa misingi ya mazingira mabovu ya kufanyia kazi.

Mashabiki pamoja na washikadau wanasubiri ngoma za binafsi kutoka kwake Queen P ili kupima ukwasi wake kati muziki ikiwa kwamba ngoma hiyo ya #pressure alimshirikisha bosi wake, Willy Paul.

 

Msanii Willy Paul amempongeza mwanamuziki Miss P , hii ni baada ya ngoma yake #Pressure kutinga views milioni moja kwenye mtandao wa Youtube.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa ameambatanisha na picha ya Miss P, Pozze amemhongera kwa kuwahi views milioni moja kwa ngoma yake ya kwanza chini ya usimamizi wa Saldido International Records.

“Kongole kwa views milioni moja katika kazi yako ya kwanza,” aliandika Willy Paul.