Jinsia yangu itasalia siri mpaka nitakapoamua kusema - Kinutha

Muhtasari

• Mfalme wa kuachia video katika mtandao wa Tiktok, Kinuthia amesema kwamba hali yake ya kimapenzi itasalia kuwa siri mpaka wakati ambapo ataamua kuweka wazi kuhusu mchumba wake.

• Akizungumza na mwanablogu Commentator 254, Kinuthia amesema kwamba anachukizwa kwa jinsi ambavyo wakenya wengi wamekuwa wakibuni mambo ya uongo kuhusu mahusiano yake, huku akisema kwamba akiwa tayari kuweka wazi kwa umma atafanya hivo bila wasiwasi wowote.

Image: TWITTER

Mfalme wa kuachia video katika mtandao wa Tiktok, Kinuthia amesema kwamba jinsia yake itasalia kuwa siri mpaka wakati ambapo ataamua kuweka wazi kwa umma.

Akizungumza na mwanablogu Commentator 254, Kinuthia amesema kwamba anachukizwa kwa jinsi ambavyo wakenya wengi wamekuwa wakibuni mambo ya uongo kuhusu jinsia yake, huku akisema kwamba akiwa tayari kuweka wazi kwa umma atafanya hivo bila wasiwasi wowote.

Kinuthia tangu awe mtu maarufu nchini, mashabiki wengi wamekuwa katika njia panda iwapo yeye ni ama mwanamke au mwanaume kwa jinsi ambayo anavaa na mitindo anayotamba nayo inayoonekana kuwa ya kisichana zaidi.

Amewaomba mashabiki kukoma kuibua madai kwamba kila mtu  anayeshirikiana naye kwenye kazi kwa muda mrefu wanatoka naye kimapenzi, akisema kwamba huwa anachukizwa sana na tabia hiyo ya mashabiki ambayo anasema imedumu kwa muda sasa.

Aidha amesema kwamba ana mapenzi mengi kwa msanii Diana B huku akikiri kwamba angependa sana kukutana naye kwani amekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu sasa.