Syokau ameibua madai kwamba Rington anampenda lakini hataki ijulikane

Muhtasari

• Justina Syokau ameibua mapya kwamba Rington anampenda nyuma ya pazia lakini anamkana mbele ya kamera kwenye watu

• Syokau anatarajia mwenyekiti wa wasanii wa injili Rington ampatie zawadi ya gari ya Mercedes Benz wakati huu wa Valentino

Justina Syokau
Justina Syokau
Image: HISANI

Mwanamuziki wa injili mwenye utata Justine Syokau almaarufu madam 2020 ameibua madai mengine tena siku hii ikiwa ni siku spesheli ya wapendanao kwamba msanii mwenza Rington anampenda lakini hataki kuliweka bayana mbele ya kamera.

Syokau ambaye ni mama wa mtoto mmoja na ambaye amekuwa bila mchumba kwa muda wa miaka tisa anasema kwamba Rington anampenda nyuma ya pazia lakini ifikapo mbele ya kamera kwenye umati, msanii huyo aliyejitangaza kuwa mwenyekiti wa wasanii wa injili anajifanya hamjui na kumkataa.

"He is my crush. Anajua nampenda na ananipenda. Behind the scenes we are in love but in front of cameras he denies knowing me. Ananiruka kipeteo kiyesu," alisema madam 2020.

Akiandika kwenye mitandao ya kijamii, msanii huyo amemshabikia Rington kwa ujumbe maalum wa mahaba

“Happy valentine Rington Alex Apoko,” ameandika Syokau

Vile vile Syokau alisema kwamba kwa vile wanapendana na Rington, anatarajia zawadi ya gari aina ya Mercedes Benz

“Nasubiria Rington kuniletea zawadi ya gari aina ya Mercedes Benz siku hii ya valentino kwa sababu siku ya kuzaliwa kwangu hakuniletea. Siwezi nikatuama kwa mambo madogo,” Syokau alisema

Mwezi jana wakati alikuwa akijiandaa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake aliibua madai mitandaoni kwamba Rington ndiye mwanaume wa ndoto zake na alitaka amzawadie gari la kifahari lakini Rington alifyata kimya madai hayo.