Simjui! - Rose Muhando akana mahusiano na Abraham Mutai

Muhtasari

• Mwimbaji mashuhuri wa injili Rose Muhando amejitokeza wazi na kukana mahusiano ya kingono na mwanablogu Abraham Mutai

• Amesema hata hana ufahamu mwanablogu huyo ni nani na kusema hamjui.

Rose Muhando

Mwimbaji mashuhuri wa injili Rose Muhando amejitokeza wazi na kukana mahusiano ya kingono na mwanablogu Abraham Mutai ambayo yalisambazwa mitandaoni mwezi uliopita na baadhi ya Wakenya.

Akizungumza katika kituo kimoja cha redio nchini, Muhando amepuuzilia mbali madai ya kufanya ngono ya usiku mmoja  na mwanablogu huyo kwenye klabu kimoja huko Thika kama ilivyosemekana. Amesema hata hana ufahamu mwanablogu huyo ni nani na kusema hamjui.

"Mimi sijali na sijutii sababu sina hatia na wala sijawai kutia unajisi katika ardhi ya Kenya. Ajipange upya sababu amefeli,” alisema Muhando

Mwezi jana, mwanamme mmoja alimtuhumu Abraham Mutai kwa kufanya ngono na Rose Muhando kwenye klabu huko Thika na kusema kwamba yeye ndiye aliwaelekeza wawili hao kwenye chumba cha kukodisha.

"Huwa sipendi kujibu tuhuma za kijinga kama hizo kwa sababu si za kweli n ani za kipumbavu. Mimi hata simjui Abraham Mutai na sijawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na yeye. Aseme tu kama ananipenda hapo sawa,” alisema Muhando.

Mwimbaji huyo amesema kwamba hata kama watu walimuona katika sehemu hiyo akikodisha chumba cha malazi hakuna tatizo kwani kila mara yeye anapokuwa nchini hukodisha chumba kwa ajili ya kulala kwani hana nyumba yake nchini Kenya.

Mwezi jana madai hayo yaliposambazwa mitandaoni, mwanablogu Abraham Mutai aliyapuuzilia mbali pia na kusema kwamba wale waliokuwa wakiyasambaza ni wenye walikuwa wametofautiana kisiasa, haswa ikizingatiwa kwamba mwanablogu huyo anatofautiana vikali na sera za naibu rais William Ruto ambaye wanatoka eneo moja la mkoa wa bonde la ufa.

“Mimi nasisitiza vikali kwamba sikuwahi lala na Rose Muhando katika chumba namba 4 mjini Thika ama mji wowote… mawakili wangu watamtembelea huyo mpokezi katika hoteli hiyo ili kubaini ukweli,” alisema Mutai.