Mpenzi wa Presenter Ali afunguka kuhusu kubadilisha dini

Muhtasari

• Mke wa mtangazaji na mwanablogu Presenter Ali, Medina ameelezea kuhusu sakata la yeye na mpenziwe kuachana nan i vipi walifanikiwa kulifufua penzi lao.

• Ametoa ushauri kwa vijana wenzake kuchukua muda wao wanapotaka kuingia katika ndoa ili kufanya maamuzi ya kibusara.

Presenter Ali
Presenter Ali
Image: Instagram KWA HISANI

Mke wa mtangazaji na mwanablogu Presenter Ali, Medina ameelezea kuhusu sakata la yeye na mpenziwe kuachana nan i vipi walifanikiwa kulifufua penzi lao.

Akizungumza kupitia video aliyopakia katika akaunti yake ya YouTube, Medina ameeleza kwamba utofauti wa dini kati yao wawili ulipelekea wao kukatisha penzi lao ambalo lilikuwa limeanza kunawiri.

Medina amesema kwamba yeye alikuwa mkiristu na ili kuolewa na Ali, alipaswa kubadilisha dini na kuwa muislamu jambo ambalo lilimtia tumbo joto kwa muda mrefu.

Baada ya kuliwazia suala hilo kwa muda mrefu na kufanya mazungumzo na mamake mzazi, Medina aliamua kubadilisha dini ili kuokoa penzi lao.

Ilimlazimu kujifunza mila na tamaduni za dini hiyo yaKiislamu  ili kukubalika na familia ya mpenziwe.

Ametoa ushauri kwa vijana wenzake kuchukua muda wao wanapotaka kuingia katika ndoa ili kufanya maamuzi ya kibusara.