Siwezi saidia kila mtu, mimi si UNICEF - Redsan awajibu wasanii chipukizi

Muhtasari

• Kwanza mnafaa kujua kwamba Redsani si UNICEF. Hii imekuwa ni trend sana kwa wasanii chipukizi wakipiga wasanii wakongwe kwenye muziki - Redsan

redsan
Redsan redsan

Msanii mkongwe wa mtindo wa dancehall Redsan amejitoa wazi wa kuwajibu wanaomsuta kwamba hakusaidia wasanii chipukizi enzi alizokuwa akitamba kimuziki.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na Watangazaji Mwende na Clemmo, Redsan aliwasuta wasanii wanaomkashfu kwamba hakuna msanii hata mmoja ambaye alishika mkono wakati alikuwa anadedea kimuziki. Redsan alisema kwamba wasanii hao wanaomsuta ni wale wazembe ambao wanataka kufanikiwa kimuziki bila kufanya bidii.

Nguli huyo alisisitiza kwamba wasanii wa siku hizi hawawezi tia bidi kimuziki nay eye akasema kwamba Kenya mahali imefikia inahitaji wasanii wanaoweza unda muziki utakaoshindana katika tuzo kubwa kama Grammy. Alisema kwamba katu hawezi saidia msanii asiyejituma kwa sababu yeye si shirika la kutoa msaada.

“Kwanza mnafaa kujua kwamba Redsani si UNICEF. Hii imekuwa ni trend sana kwa wasanii chipukizi wakipiga wasanii wakongwe kwenye muziki. Wasanii wa kitambo si UNICEF, acha wasanii wajitokeze ili washindane na sisi wote, mkijituma mtainuka. Kuna njia moja tu na kufanikiwa, kufanya bidii. Kama uko na shida na matamshi yangi basi uko na shida,” alisema Redsan.

Itakumbukwa huyu ni msanii wa pili baada ya mbunge wa Starehe Jaguar kujitoa wazi na kuwapa changamoto wasanii wa Kenya kutoa muziki mzuri na ambao unaleta maana.