Ponda raha mpenzi wangu wa zamani, maisha ni mafupi - Eudoxie amwambia Grand P

Muhtasari

• Eudoxie Yao amemtakia Grand P kila la kheri katika maisha baada ya video ya mwanamuziki huyo akiogelea na mwanamke mwingine

Image: INSTAGRAM// GRAND P

Mwanamitindo mwenye mwili mkubwa kutokea nchini Ivory Coast Eudoxie Yao amemtakia kila la kheri katika maisha aliyekuwa mpenzi wake Grand P, baada ya kumuona kwenye video akijivinjari katika kwenye bwawa la kuogelea na mwanamke mwingine.

Katika video hiyo, mwanamuziki huyo kutoka Guinea mwenye umbule dogo Zaidi la mwili amepakia video hiyo wakiogelea kwenye Facebook yake na kusema kwamba anajivinjari kadri ya uwezo wake kwani Maisha ni mafupi mno.

“Maisha ni kitu cha kuvutia sana, jibambe kadri ya uwezo wako. Mimi najivinjari kivyangu,” aliandika Grand P

Katika sehemu ya kutoa maoni, aliyekuwa mpenzi wangu ambaye pia ni mwanamitindo Eudoxie Yao ameandika ujumbe wa kumtakia kila la kheri anapojibamba katika Maisha.

Facebook

“Jibambe mpenzi wangu wa zamani, Maisha ni mafupi,” aliandika Eudoxie Yao.

Fununu za kuachana kwa wawili hao zilizuka wakati wa mashindano ya AFCON nchini Cameroon mapema mwezi Februari wakati mwanaume huyo mdogo alionekana akiwa na wanawake wengi wakisherehekea ngarambe hiyo, jambo linalotajwa kumkera Yao na kumpelekea kufanya maamuzi ya kumuacha Grand P.