Rayvanny apokea ubalozi PM Bet

Muhtasari

• Msanii kutoka lebo ya WCB Wasafi, Rayvanny ameteuliwa kama balozi wa kampuni ya kubashiri ya PM Bet February 19.

• Uteuzi huu umezua hisia mseto kutoka mashabiki wa Wasafi ambao pia wanashabikia kampuni ya ubashiri ya Wasafi Bet

Rayvanny
Image: HISANI

Msanii kutoka lebo ya WCB Wasafi, Rayvanny ameteuliwa kama balozi wa kampuni ya kubashiri ya PM Bet February 19.

Msanii huyo ambaye anapokea ubalozi kwa mara ya kwanza amewashukuru wote wakiwemo wanahabari na pia kampuni ya PM Bet kwa kumuaminia na ubalozi wa brand yao.

“Niishukuru sana PM Bet kwa kuniamini na kuona kwamba naeza nikasimama kwenye brand ya PM Bet na kuipa value na kuona kwamba tunasongea mbele na kuendelea kuenda mbali Zaidi. Hii ni endorsement yangu ya kwanza kwa sababu nyingi zimekuwa zikija lakini tumekuwa tunavutana sana kwa kuwa mimi ni mtata sana katika mambo ya hela,” alisema Rayvanny.

Kampuni ya kubashiri ya PM ina miaka minane katika soko la ubashiri na msanii huyo ameisifia kuwa kampuni mahiri inayojua chenye wanafanya kwa ustadi mkubwa.

Hili limezua hisia mseto kutoka wafuasi wake na haswa wale wanaomfuatilia kutoka lebo ya Wasafi ambayo inaongozwa na msanii Diamond ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kubashiri ya Wasafi Bet ambayo ilizindulia miezi miwili iliyopita.

Wengi wanahisi kwamba msanii Rayvanny hangepokea ubalozi wa PM Bet kwa sababu ni kampuni inayoshindana na Wasafi Bet kwenye masoko ya ubashiri na tukio hili limetajwa na wengi kuwa ni usaliti kwa Wasafi ambapo wengi wanahisi angeipigia upato Zaidi Wasafi Bet na si PM Bet.

Ila pia baadhi wanahisi msanii Rayvanny amekomaa sasa n ani jambo la busara kukubali ubalozi kutoka kampuni yoyote hata kama kampuni hiyo ina ushindani wa aina yoyote ile na kampuni zinazohusishwa na bosi wake Diamond Platnumz, n ani vizuri aendelee kusukuma brand yake kama Rayvanny chini ya lebo yake ya Next level Music pasi na kuwekewa vikwazo vya kibiashara na kimikataba na kampuni mzazi, nazungumzia WCB Wasafi.

Ikumbukwe uteuzi huu unakuja siku chache tu baada ya habari kuzagaa mitandaoni kwamba Rayvanny anataka kuondoka Wasafi kabisa ila amefungiwa na baadhi ya vipengele katika mkataba wake wa awali na lebo hiyo, na kwamba hana furaha kabisa na vipengele hivyo ambavyo havikuwekwa wazi.

Je, maoni yako ni yepi kuhusiana na msanii huyo kuteuliwa kama balozi wa PM Bet ambayo inapigania nafasi kwenye soko la ubashiri na Wasafi Bet?