Mcheza santuri wa ngoma za Mugithi nchini Kenya DJ Faxto amekuja na jipya tena, wiki moja tu baada ya kuwakabidhi wazazi wake nyumba aliyowajengea.
Safari hii mcheza santuri huyo amemrushia bonge la surprise mpenzi wake kwa kumnunulia gari alipokuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Akimsherehekea kwenye siku yake spehseli ya kuzaiwa, Faxto amemsifia mpenzi wake kwa kusimama na yeye wakati alikuwa anateseka kimaisha.
“Watu jamani nisaidie kumtakia mwanadada huyu mwenye roho nzuri kheri njema za kuzaliwa. Nilijiwekea ahadi mimi mwenyewe kwamba nitarudi kwa wale wote waliosimama upande wa Faraja yangu wakati nilikuwa nateseka,” aliandika Faxto kwenye Instagram yake.
Pia mcheza santuri huyo ambaye pia ni mwanamuziki alimwambia mpenzi wake kwamba ajibambe na zawadi hiyo ya gari ila asisahau kumuombea mwanaume wake, ambaye ni yeye mwenyewe.
“Sherehekea na hii mashine mpya ya kwako na usisahau kumuombea mpenzi wako,” aliandika Faxto.
Zawadi hii kwa mmoja kati ya watu anaowataja walisimama upande wa Faraja yake wakati jua, kiangazi, mvua na kipupwe vilikuwa vya kwake, inakuja wiki moja tu baada ya Faxto kuwakabidhi wazazi wake nyumba aliyowajengea na kuwasherehekea siku ya Valentino kwa kuwa wazazi wema kwake.
Siku ya Valentino, mcheza santuri huyo aliwasherehekea wazazi wake kwa kumfunza maadili mem ana kudokeza kwamba mafanikio yake kwenye Maisha yalikuwa yamechangiwa pakubwa na wazazi wake.