Baada ya kufana AFRIMA, Nikita Kering atuzwa tena PMVA

Muhtasari

• Nikita Kering ameshinda tuzo za PMVA miezi mitatu tu baada ya kuwapiku Nandy na ZXuchu na kuibuka mshindi wa AFRIMA, kitengo chqa mwanamuziki bora Afrika Mashariki.

Nikita Kering
Image: INSTAGRAM

Msanii Nikita Kering anaendelea kuvuna pakubwa katika Sanaa ya muziki ndani na nje ya Kenya kwa juhudi zake kubwa anazoziweka kwenye Sanaa.

Baada ya kuwapiku wasanii tajika kama Nandy na Zuchu katika tamasha la AFRIMA mwezi Novemba mwaka jana na kuibuka mshindi wa tuzo hiyo ya mwanamuziki bora wa kike kutoka Afrika mashariki, Nikita hakulaza damu kwani aliendelea kutia bidi na Alhamisi 24 Februari, mwanamuziki huyo alituzwa katika hafla ya PMVA jijini Nairobi kwa video bora yam waka 2021.

Mwanadada huyo anazidi kuzivamia tuzo mbalimbali ndani na nje ya Kenya kwani mwezi Novemba, Kering alishinda tuzo mbili za AFRIMA, moja ya kuwa msanii bora wa kike kutoka Mashariki mwa Afrika na ya pili ikawa ni Mwanamuziki bora wa mitindo ya RnB na Soul.

Katika tuzo za Pulse Music Video Award zilizoandaliwa mgahawani Nairobi Street Kitchen, Kering alituzwa kwa video bora ya kike na kuwahukuru wafuasi na mashabiki wake wote kwa kumuaminia na kumpigia kura.

“Ahsante kwa kupiga kura, Female video of the year,” aliandika Kering kwenye Instagram yake.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 20 amekuwa akishinda tuzo mbalimbali kwani kwake imekuwa mazoea kutokana na bidi kubwa kimuziki. Mwaka 2019, Kering pia alishinda tuzo za AFRIMA na kuwashukuru wasimamizi kwa kumtambua, kumteua na baadae kushinda.

Hongera sana Nikita Kering.