logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nandy afumaniwa na Mwijaku, akana madai ya kuchepuka

Mwijaku amemfumania Nandy akidhani anachepuka, ikabidi adhibitishe kutoka kwa Billnass.

image
na Radio Jambo

Makala01 March 2022 - 07:31

Muhtasari


• Mwijaku amemfumania Nandy usiku kwenye shoot akadhani anachepuka na ikabidi adhibitishe kutoka kwa mpenzi wake Billnass.

Mwanamuziki wa bongo fleva, Nandy amekanusha madai kwamba anachepuka baada ya mtangqazaji wa shirika la habari la Clouds kumfumania usiku akizindikizwa kwenye gari na mwanaume mwingine ambaye Mwijaku alibaini si yule ambaye amemchumbia juzi, Billnass.

Baada ya Mwijaku kumkuta akifunguliwa lango, alimzaba na maswali mazito ambapo Nandy alijikaza kujitetea kwamba yeye hachepuki na kusisitiza kwamba anajua ni mke wa mtu na pia kusema kwamba mumewe mtarajiwa anajua kwamba alikuwa sehemu hiyo katika harakati za kufanya video.

“Mwijaku mimi ni mke wa mtu, niko kwenye shooting na mume wangu anajua. Usinitafutie matatizo na nampigia simu sasa hivi adhibitishe,” Nandy anaonekana akijitetea.

Mwijaku alidadisi kwamba tqangu lini shooting ifanywe usiku kama huo wakati anagunguliwa lango na ikabidi amshrutishe Nandy kumpigia simu Billnass.

Billnass baadae alipokea simu na kudhibitisha kwamba alikuwa na habari ya kule ambako Nandy alikuwa na hapo angalau Mwijaku akakubali na kuwaacha waendelee na shughuli yao ya shooting.

“Nimemkuta sehemu Billnass, unajua kama yuko hapa sasa hivi? Unajua eh? Hapo sawa maanake nimeogopa nimekuta nyuma ina geti kali nyumba ina walinzi halafu nikaona kuna mwanaume alikuwa anamsindikiza ndio maana nikaogopa. Basi nashukuru, nimejiakiki kumbe kweli alikua anafanya kazi,” anasikika akisema Mwijaku.

Wiki jana Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba nyumbani kwao Nandy, Mlandizi na wawili hao wakafichua kwamba ndoa rasmi haitopita mwezi wa sita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved