logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akuku Danger: Ngojeni 'first born' ndio muamini Sandra ni mpenzi wangu

Akuku Danger adhibitisha Sandra ni mpenzi wake, siku chache baada ya Dacha kusema.

image
na Radio Jambo

Makala03 March 2022 - 09:05

Muhtasari


• Akijibu maswali ya wafuasi wake kwenye Q&A ya instagram, Akuku Danger alisema wale wanashuku mahusiano yake na Sandra Dacha wasubiri mtoto wa kwanza ndio waamini.

Sandra Dacha almaarufu kama Silprosa na mpenzi wake Akuku Danger

Mcheshi Akuku Danger amewaambia wale wanaoshuku mahusiano yake na mcheshi mwenzie Sandra Dacha kwamba kama wanafikiria ni kiki wawili hao wanafukuzia mitandaoni basi wasubiri mtoto wa kkwanza ndio waamini.

Akiongea na wafuasi na mashabiki wake kweye Q&A kwenye Instagram yake Jumatano usiku, Akuku aliulizwa kama ni kweli wako katika mahusiano na Sandra Dacha ama ni mbwe mbwe za mitandaoni tun aye akajibu kwa kuashiria kwamba fununu za mapenzi yao ni kweli kwani aliwataka wanaoshuku kusubiri mtoto wa kwanza ili waamini.

“Mko katika mahusiano ya kimapenzi na Sandra Dacha ama ni ucheshi tu?” mmoja wa mashabiki aliuliza.

“Ngojeeni first born ndio uamini,” alijibu Akuku Danger.

Pia aliashiria kwamba anapanga kumuoa Dacha na kuwa na watoto naye na si kumchezea tu katika mahusiano kama ambavyo wamekuwa wakifanya wqacheshi wengi.

“Unapanga kuoa mashine yako kubwa Sandra Dacha na kuwa na watoto naye” shabiki mwingine aliuliza.

“Inshallah!” alijibu Akuku Danger kwa kuashiria kwamba majaaliwa ya Mungu hilo litafanyika.

Sandra Dacha ndiye aliyebainisha wazi kwamba Akuku Danger si Rafiki tu bali ni mpenzi wake pia na ndio maana alikuwa mstari wa mbele kuchangisha na kuitisha misaada kutoka kwa watu mbalimbali ili kugharamia matibabu ya Akuku Danger ambaye alilazwa kwa Zaidi ya mwezi mmoja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved