Eric Omondi afanyiwa maombi na wahubiri, ndiko kuokoka?

Muhtasari

• Video ya Eric Omondi akifanyiwa maombi imesambaa mitandaoni huku wengi wakigawanyika kwa maoni.

• Wengine wanadai ameokoka huku wengine wakisema ni sarakasi zake za kawaida ambazo hazitabiriki.

Eric Omondi
Image: Instagram

Huenda mchekeshaji Eric Omondi ameokoka sasa na kuacha vitimbi visivyo na stara kama ‘Wife Material’. Hii ni baada ya video yake akifanyiwa maombi ya nguvu na yenye upako uliotukuka kusambaa mitandaoni.

Katika video hiyo ambayo hadi Eric Mwenyewe ameipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, mchekeshaji huo anaonekana akiwac amepiga magoti chini na kuzingirwa na wahubiri Zaidi ya kumi hivi kama macho hayadanganyi ambapo wanasikika wakimuombea na kufukuza mapepo kutoka kwake wakisema kwamba shetani amejaribu kumnyakua lakini ameshindwa.

Eric alisema kwamba tukio hilo ambalo ameliita kama kitu cha ajabu kutokea kwenye maisha yake ilitokea katika hafla ya mazishi ya binti wa mhubiri wake huko Kitale katika kaunti ya Trans Nzoia ambapo maaskofu mashuhuri nchini Kenya walimuita na kumuwekea maombi matakatifu ambapo aliyahisi mpaka kusema Amina.

“Leo nilihudhuria mazishi ya bintiye mhubiri wangu Martin Mbandu huko Kitale ambapo tukio la ajabu lilinipata. Maaskofu wote mashuhuri nchini Kenya waliniita na kuzungumza maombi matakatifu kwa maisha yangu ambapo nilisema Amina,” aliandika Omondi kwenye Instagram yake.

Tukio hilo limepikelewa kwa hisia mesto na watu mitandaoni baadhi wakisema sasa ameokoka na kuacha sarakasi zake za kupiga picha nusu uchi huku wengine wakisema huenda hii ni moja kati ya vitimbi vyake tu ambapo anafanyiwa maombi kama moja ya maandalizi ya sehemu ya nne ya kipindi chache cha Wife Material ambayo alisema inaanza mwezi wa nne na safari hii haitashirikisha wanadada kutoka Afrika bali atatafuta Wachina, Wamarekani, Waarabu na wengine kutoka nje ya bara la Afrika.

Hebu itizame video hiyo ya Omondi hapa chini na utoe maoni yako.