logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ninapomtaka nampata tena,'Fahyvanny amshambulia Paula Kajala

Aidha msanii huyo alisema kwamba yeye na mtoto wake hawakosi chochote.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri06 March 2022 - 06:51

Muhtasari


  • Fahyvanny waliachana na msanii huyo mapema mwaka jana, na wamekuwa wakishirikiana kumlea mtoto wao

Fahyvanny ambaye ni baby mama wake staa wa bongo Rayvanny, wamekuwa wakishambuliana na Paula Kajala kwenye mitandao ya kijamii.

Fahyvanny waliachana na msanii huyo mapema mwaka jana, na wamekuwa wakishirikiana kumlea mtoto wao.

Kupitia kwenye ukurasa wa instagram wa Paula Kajala alidai kwamba yuko tayari kumletea mwanawa Rayvanny dadayake, na kudai kwamba huyo ni mwanawe.

Huku Fahyvanny akijibu madai hayo alisema kwamba akimtaka Rayvanny amrudie anaweza kwani ni baba ya mtoto wake kwa hivyo awache kujigamba sana.

Aidha msanii huyo alisema kwamba yeye na mtoto wake hawakosi chochote.

"Mwambieni uyo chai jaba Hakuna Mtu mwenye time na maisha yao nipo bize na maisha yangu na Mtoto wangu Hakuna kitu tunakosa na anaeringa nae Ni mzazi mwenzangu so ninapomtaka nampata Tena kwa wakati maana naona nikikaa kimya anataka kunipanda kichwani😏."

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved