Drake anunua jumba lenye thamani ya dola 85M za Kimarekani

Muhtasari

• Drake amekuwa gumzo la mitandaoni baada ya kununua jumba la kifahari lenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 85 ambalo lina vyumba vya kulala 10, bafu 22 miongoni mwa sehemu nyingine nyingi.

Mwanamuziki DRAKE
Mwanamuziki DRAKE
Image: Hisani

Staa wa Hip Hop, Drake sasa hivi ndiye gumzo la mitaani nchini Marekani na kote duniani kwa kununua bonge la jumba la kifahari lenye takriban kila kitu ambacho mtu wa wastani anatamani kumiliki.

Drake ambaye alishika nambari nne kwa wasanii wa hiphip waliotengeneza michuzi mingi Zaidi kwa mwaka wa 2021 kutokana na kazi zake za muziki kwa kujitilia kibindono Euro milioni 50 ametangaza wikendi iliyopita kwamba hatimaye amefanikiwa kumiliki kwa kununua nyumba hiyo yenye thamani ya kiasi cha dola za Kimarekani milioni 85.

Nyumba hiyo ambayo inapatikana katika jimbo la Los Angeles, mtaani Beverly Hills linatajwa kuwa pana Zaidi ambapo taarifa za burudani kutoka tovuti mbalimbali nchini Marekani zinaripoti kuwa ukubwa wake ni wa futi 25,000 mraba.

Jumba hilo linalofananishwa kama kasri vile linasemekana kuwa na vyumba vya kulala kumi, vyumba vya kukogea ama ukipenda bafu ishirini na mbili, maegesho ya magari kumi na moja, gym, kiwanja kidogo cha mchezo wa tenisi miongoni mwa sehemu nyingine nyingi, zote ndani ya mjengo huo huo mmoja.

Sanaa ya kimataifa ina hela wanetu, humu nchini ni kuiga tu!