Sijui natumia pesa ngapi, muhimu ni 'kuenjoy' - Irene Uwoya

Muhtasari

• Mwanamitindo Irene Uwoya anadai hajawai kadiria kiasi cha pesa ambazo anatumia katika ziara zake, cha muhimu kwake ni kujiburudisha.

Irene Uwoya
Image: Ireneuwoya/INSTAGRAM

Ukisikia pesa mfano wa njugu, basi kwa muigizaji na mfanyibiashara Irene Uwoya umegona ndipo.

Mwanamitindo huyo maarufu nchini Tanzania amewaacha wengi vinywa wazi na macho kuwatoka kodo alipozungumza na gazeti moja nchini moja na kukiri kwamba yeye hajawahi weka hesabu ya pesa anazozitumia na hata hajui ni ngapi anatumia kwa siku kwani lengo lake kuu ni kujivinjari na kujifurahisha bila kujali ni kiasi kipi kinagharimika.

Aliulizwa uwezo wake wa kugharamikia matumizi ya timu kubwa ya watu wanaotembea nao na kuonekana kwenye picha katika migahawa mbalimbali yenye hadhi ya nyota tano na akasema kwamba huwa inategemea tui la kikubwa na ambacho anakijali yeye ni kujiburudisha maishani.

Uwoya anajulikana na wengi kwa maneno yake ambayo aghalabu hupenda kuyasema kwamba yeye huwa hatafuti pesa wala huzitega tu na zinaingia zenyewe kwenye kitonga.

Mara nyingi huwa siwezi kujua ni kiasi gani cha pesa kwa sababu huwa sipendi kuongelea sana hilo suala kwamba eti natumia kiasi gani, inategemea na bata lenyewe linafanyikia wapi,” alijibu Uwoya.

Hii inakuja siku chache tu baada ya msanii Noti Flow kutoka Kenya kudai kwamba kwa wiki yeye hutumia kiasi cha Zaidi ya milioni moja za Kenya, tamko ambalo liliwaacha wengi katika mshangao mkubwa.

Aisee! Watu wako na pesa, ukisema hakuna pesa jua umesimama peke yako.